MAKOSA YA KISARUFI NA KIMANTIKI KATIKA LUGHA - Printable Version +- JIFUNZE KISWAHILI (https://jifunzekiswahili.co.tz) +-- Forum: My Category (https://jifunzekiswahili.co.tz/forumdisplay.php?fid=1) +--- Forum: Sarufi na Utumizi wa lugha (https://jifunzekiswahili.co.tz/forumdisplay.php?fid=9) +--- Thread: MAKOSA YA KISARUFI NA KIMANTIKI KATIKA LUGHA (/showthread.php?tid=1601) |
MAKOSA YA KISARUFI NA KIMANTIKI KATIKA LUGHA - MwlMaeda - 11-28-2021 MAKOSA YA KISARUFI NA KIMANTIKI KATIKA LUGHA
Pale lugha inapotumika tofauti na malengo hupoteza lengo na madhumuni ya mzungumzaji kwa msikilizaji wake. Upotoshaji huu hujitokeza katika sarufi au mantiki.
MAKOSA YA KISARUFI
Kila lugha ina kanuni na taratibu ambazo hutawala katika matumizi ya lugha ili watu waweze kuelewana kanuni hizo zinapovunjwa au kukiukwa huweza kusababisha makosa kujitokeza na upotovu katika lugha. Makosa ya kisarufi yanaweza kugawanyika katika sehemu zifuatazo:-
Makosa ya kimsamiati
Watumiaji wa lugha huchanganya masamiati wakati wa kuzungumza au kuandika. Watu hutumia msamiati usiolingana na msamiati usiolinga na maana iliyokusudia
Mfano:- Nona na nenepa
Wengi husema siku hizi umenona sana.
Badala ya kusema, Siku hizi umenenepa sana.
mazingira na mazingara
Watu husema Mazingara yameharibiwa sana siku hizi.
badala ya kusema Mazingira yameharibiwa sana siku hizi.
Ajali na ajili
Watu husema Amefariki wa ajili ya gari.
badala ya kusema Amefariki kwa ajali ya gari.
Wakilisha na wasilisha
Watu husema, Waziri wa fedha atawakilisha bajeti ya mwaka kesho.
Badala ya kusema Waziri wa fedha atawasilisha bajeti ya mwaka kesho.
Makosa ya kimuundo
Kwa kawaida sentensi za kiswahili huanza na nomino ya mtenda au mtendwa.
Mfano:- mtoto mpole anacheza
Mzungumzaji asiye fuata kanuni husema Mpole mtoto anacheza.
Kalamu yangu imeibwa.
badala ya kusema kalamu yangu imeibiwa.
Makosa ya kimatamshi
Watu wengi hushindwa kutamka baadhi ya sauti za kiswahili wakati mwingine huchanganya na kubadili sauti hizo Mfano Wakurya hutumia ’r’ badala ya ’l’
Nenda karare
badala ya kusema nenda kalale
Wandali hutumia ’s’ badala ya ’z’ na ’dh’ na ’th’
mfano selasini
badala ya thelathini
Sahabu
badala ya dhahabu
Samani
Badala ya zamani
Makosa haya mara nyingi yanatokana na athari ya lugha mama. Kwa kuwa lugha ya kiswahili ni lugha ya pili kwa wazungumzaji wengi. Hivyo lugha ya kwanza huwa na athari kubwa kwa mzungumzaji wa wa lugha ya pili.
Kosa la kuongeza vitamkwa
Baadhi ya wazungumzaji huongeza vitamkwa mahari pasipo hitajika na hivyo kuharibu lugha.
Mfano. Nendaga
badala ya nenda
Mashule
badala ya shule
Huwaga anapenda fujo
badala ya huwa anapenda fujo
Kosa la kuacha maneno
Watumia lugha huweza kuacha maneno katika sentensi na bado wakafikiri wanatoa ujumbe uleule uliokusudiwa.
mfano, Watu husema Juma ameondoka kazini akiwa na maana kuwa Juma ameondoka kwenda kazini lakini sahihi ni kuwa Ametoka kazini.
Alfredi amerudi kazini akiwa na maana kuwa Afredi ametoka kazini.
Kwa mzungumzaji anatoa maana ambayo ni kinyume kabisa na ile maana aliyo kusudia kusema. Ambapo anakusudia kuuliza kama Alfredi amekwenda tena kazini.
Makosa ya tafsiri sisisi
Tafsiri sisisi ni tafsiri ya neno kwa neno. Tafsiri hii inapofanywa huleta matatizo ya kisarufi katika lugha
mfano. Kimbizwa hospitali
She runed to hospital
badala ya kusema amepelekwa hospitali
At the end of the day
Mwisho wa siku.
Badala ya kusema hatimaye.
MAKOSA YA KIMANTIKI
Mantiki ni utaratibu mzuri wa kufikiri. Makosa ya kimantiki ni yale yanayoonesha kukosekana kwa utaratibu wa fikra. Nimakosa yanatokana na upotovu wa mawazo ya mzungumzaji.
Mfano; watu wengi husikika wakiema hivi: Usimwage kuku kwenye mchele mwingi
Badala ya usimwage mchele kwenye kuku wengi
Nyumba imeingia nyoka
Badala ya kusema Nyoka ameingia ndani ya nyumba
Chai imeingia nzi
Badala ya kusema Nzi ameingia kwenye chai.
KUSAHIHISHA MAKOSA
Katika lugha yeyote ile makossa ya kawaida yataendelea kuwepo kama ilivyo katika lugha ya Kiswahili, kwa hiyo hatuna budi kujitahidi kusahihisha na kuzuia makosa hayo.
Watumiaji wa lugha inawabidi kuhakikisha makosa ya kisarufi na kimantiki katika msamiati, matamshi, muundo na maana hayaendelei kujitokeza kwenye mazungumzo, barua, shuleni na hata kwenye vyombo vya habari kama vile Magazeti, redio na televisheni.
Jambo la muhimu ni lazima jitihada za marekebisho ya kisarufi na kimantiki zitiliwe mkazo tangu kiwango cha elimu ya shule ya msingi, sekondari na vyuoni hadi vyuo vikuu.
Mara kadhaa makosa ya kimsamiati yamekuwa yakisababishwa na vyombo vya habari kwa hiyo ni muhimu somo la matumizi wa lugha ya Kiswahili lizingatiwe vyema katika vyombo vyote vya habari ili kuepusha upotoshaji wa lugha.
Kwa sababu hiyo kamusi inabaki kuwa kitabu muhimu sana kwa sababu huwa na orodha ya maneno mbalimbali yanayotumiwa na wazungumzaji wa lugha na maana zake.
|