VIAMBISHI NYAMBUAJI NA VINYAMBUAJI VYA KILEKSIKA - Printable Version +- JIFUNZE KISWAHILI (https://jifunzekiswahili.co.tz) +-- Forum: My Category (https://jifunzekiswahili.co.tz/forumdisplay.php?fid=1) +--- Forum: Sarufi na Utumizi wa lugha (https://jifunzekiswahili.co.tz/forumdisplay.php?fid=9) +--- Thread: VIAMBISHI NYAMBUAJI NA VINYAMBUAJI VYA KILEKSIKA (/showthread.php?tid=1586) |
VIAMBISHI NYAMBUAJI NA VINYAMBUAJI VYA KILEKSIKA - MwlMaeda - 11-28-2021 Jinsi ya kushughulikia viambishi nyambuaji na vinyambuaji vya kileksika katika Kamusi. Ilioneshwa hapojuu kuwa viambishi nyambuaji vitazamwe kama leksimu kama ilivyo kwa mofimu nyingine ambazo siyo. Matokeo yake ni kwamba upangaji dhahiri wa faridi nyambuaji katika kamusi unahitaji pia upangaji bainifu na sisisi wa viambishi nyambuaji ili kuwezesha kutoa taarifa halisi juu ya vipengele vya kisintaksia, vya kileksika na vya kisemantiki vya faridi nyambuaji. Kwa hiyo, jitihada ya kufafanua mofolojia ya uambishaji haina budi kuchukulia viambishi nyambuaji kama msingi wa uundaji wa maneno mapya. Vinyambuo vitokanavyo na uambishaji wa nomino vinaweza kutolewa kama vitomeo huru kama ilivyokuwa katika Kamusi ya Kiswahili, lakini viambishi nyambuaji vikiwa vimechapwa katika alama maalum kama herufi za italiki. Maelezo dhahiri kuhusu unyambuaji, wa maneno yatoiewe katika utangulizi wa Kamusi. Kitomeo cha nomino nyambuaji kitakuwa kama ifuatavyo:
(28) m- sem- aj-i n.k.
Msingi wa uundaji wa vitenzi ni uambishaji wa viambishi tamati. Viambishi nyambuaji vya vitenzi ndivyo vinavyofanya kazi hiyo. Kila kiambishi tamati kitachukuliwa kama leksimu pamoja na kitomeo chake pekee. Pia itakuwa vizuri kuorodhesha chini ya kila kitomeo viambishi tamati vyote vinavyoweza kujitokeza na umbo hilo na kuunda neno jipya. Kwa mfano, chini ya som-a, viambishi tamati -w-, esh-, -ek-, -e- n.k vitaorodhesha. Lakini ikumbukwe kuwa kila unyambuaji unatoa leksimu mpya. Kutokana na hali hiyo ni muhimu kubadili kabisa jinsi ya kuandaa Kamusi ya Kiswahili. Majina yangeorodheshwa pamoja na viambishi vyao, vitenzi na viambishi viorodheshwe kwa msaada wa mashina yao na viambishi nyarabuaji vitaorodheshwa kiutaratibu wa sisisi kama leksimu tofauti. Viambishi nyambuaji vyote vitatofautishwa na faridi nyingine zisizo viambishi kwa kuvichapisha kwa alama pekee (k.v. italiki k.m.). Lakini kwa sasa mpangilio wa vitomeo katika Kamusi ya Kiswahili Sanifu utaendelea lakini pamoja na mabadiliko kwa kuzingatia nafasi ya uambishaji na unyambuaji. Baadhi ya mapendekezo yetu ni kama yafuatayo:
(a) Kwanza, ingefaa viambishi vyote viandikwe kwa chapa tofauti na mzizi asilia wa neno ili kubainisha leksimu
(b) Kuhusu vitenzi. mzizi na irabu ya mwisho wa kitenzi kwa chapa ya pekee iliyo tofauti na ile ya viambishi nyambuaji. Katika kitenzi, mzizi wamsingi ni ule ambao ukiunganishwa na irabu ya mwisho ya kitenzi unatoa maana ya msingi ya kitenzi hicho. Irabu ya mwisho kwa hiyo itabidi isiambatishwe na kiambishi au sehemu yoyote ya kiambishi tamati nyambuaji, k.m Nomino
(29) m tu
m-som-i m-som-aj-i tunda/ma-tunda n.k. Vivumishi (sifa) Mashina tu ya vivumishi vya sifa yataingizwa yakitangutiwa na kistari kama kivumishi husika kmapatanishwa kisarufi, k.m. (30)- kubwa
– refu lakini hodari n.k. Vitenzi Itakumbukwa kwamba katika Kiswahili irabu za mwisho za vitenzi visoukomo ni zifuatazo:
(31)
-a
-kat-a
– u
-abud-u
– i
-fik-i
– e
-stareh-e
Tuliona umuhimu wa kuchambua kwa kina mfumo wa mizizi ya vitenzi na wa viambishi nyambuaji vya Kiswahili. Hapa tutatoa tu kwa mifano baadhi ya mapendekezo yetu juu ya kushughulikia masuala hayo.
(32)
-kat-
-kat-ish -a-a
ahir –
-kat-an-a
fung-
-kat-w-a n.k
-fung-a
-ahiri-ish-a
-fung-i-a
-erevu-erevu-k-a
-fung-ish-a
-fung-an-a
-fung-u-a
-fung-aw-a
an-a n.k.
Unyambuaji wa maneno kutoka Kiarabu ufanyiwe uchunguzi ili wasomaji wa kamusi waelewe kanuni zilizotumika.
Mifano:
idara f mudiri / mudiria
abiria / abiri ibada / abudu ridhaa / ridhi Katiba/ katibu/mkataba/maktaba/mkutubi/ kitabu. karimu/kirimu maliki/malkia ridhika/mtaaridhi tabibu/tibu/matibabu Tunajiuliza pia kuwa sta- na ta- ni viambishi au vipi k.m.
m – staarabu/ mwarabu!4 stashahada/shahada stakabadhi/? kabidhi tadaraki / madaraka tabibu /matibabu tafakari/fikiri tafaraji /faraja tahariri/kuhariri taratibu/ratibu n.k. Katika (mantiki hiyo, je tunaweza kupata jozi za aina ya:
* Mstaafrika/mwafrika? * Mstazungu/mzungu? Hitimisho Tumeona kwamba vipengele vya kisarufi katika kamusi vinahusu uambishaji na unyambuaji katika uundaji wa maneno. Tumeona pia kuwa tatizo mojawapo la watunga kamusi za Kiswahili linatokana na kutofanya utafanuzi wa kina kuhusu mofolojia ya viambishi vya Kiswahili. Imebainika pia kuwa uundaji wa majina na vitenzi katika Kiswahili unashughulikiwa vizuri sana katika leksimu ambapo kanuni za kileksika zinazotawala viambishi nyambuaji zitadhihirishwabayana. Kwa sababu hizi uundaji wa maneno na wa vitenzi vya Kiswahili ni suala la kileksika. Kutokana na hali hiyo utaratibu wa kuandaa Kamusi ya Kiswahili hauna budi ubadilishwe ili viambishi nyambuaji viingizwe kama vipashio vya kileksika pamoja na vitomeo vyao pekee katika kamusi.
Biografia
1. DUBOIS, J. na wengine 1973. Dictionare de linguistique, Paris, Librarie,
2. Taasisi ya Uchunguzi wa Kiswahili 1981. Kamusi ya Kiswahili Sanifu, Dar es Salaam: Oxford University Press.
3. BOUQUIAUX, L. na TOMAS, J.M.C. 1976. Enquete et description de langues a tradition orole. Vol. 1 L’ Enquete de terrain et l’ analyse grammaticale. Paris: SELAF. 2 ed, 258 p.
4. POLOME, E.C. 1967. Swahili Language handbook. Washington: Center for Applied linguistics 232 p.
5. KAPINGA, M.C. (Mtayarishaji) 1983. Sarufiya Maumbo ya Kiswahili Sanifu. Dar es Salaam, Taasisi ya Uchunguzi wa Kiswahili.
6. NKWERA, F.M.V. 1985. Sarufi na Fasihi Sekondari na Vyuo. Dar es Salaam: TPH.
7. Taasisi ya Uchunguzi wa Kiswahili, ISTILAHI (Isimu) mswada ambao haukuchapishwa.
8. BWENGE, M C.M.T., “Affixional Morphology and Dictionary design with particular reference to Swahili lexicography” (Unpublished) Exeter University. |