MATATIZO YA UCHAMBUZI WA MOFIMU - Printable Version +- JIFUNZE KISWAHILI (https://jifunzekiswahili.co.tz) +-- Forum: My Category (https://jifunzekiswahili.co.tz/forumdisplay.php?fid=1) +--- Forum: Sarufi na Utumizi wa lugha (https://jifunzekiswahili.co.tz/forumdisplay.php?fid=9) +--- Thread: MATATIZO YA UCHAMBUZI WA MOFIMU (/showthread.php?tid=1585) |
MATATIZO YA UCHAMBUZI WA MOFIMU - MwlMaeda - 11-28-2021 MATATIZO YA UCHAMBUZI WA MOFIMU Maneno yaliyo mengi katika lugha yanaweza kukatwakatwa katika mofimu zinazohusika, lakini yapo baadhi ambayo hayaingii kwa urahisi katika utaratibu unaojulikana, yaani hayakubali kufuata kanuni zilizo wazi. Yafuatayo ni baadhi tu ya mapengo yanayojitokeza katika kuainisha mofimu za maneno ya Kiswahili.
Mofimu za umoja na wingi katika baadhi ya ngeli za nomino zinatatiza katika uainishaji wao, kwa mfano katika maneno yafuatayo:
a) chungwaa1) machungwa
b) bega
b1) mabega
c) jiwe
c1) mawe
Maneno yote haya ni ya ngeli za 5/6, lakini tukiangalia mofimu ya umoja tunaona kuwa katika (a,b) hakuna umbo dhahiri la mofimu hiyo, ambapo katika © umbo linalojitokeza ni /ji/. Tuseme nini basi, kuhusu uainishaji wa maneno {chungwa, bega} ili tuweze kuyahusisha na {jiwe}? Tuyaainishe kama mofimu mbili mbili, yaani Idambishi-ngeli na mzizi? Tukifanya bivyo, ni lazima tuseme kuwa mofimu ya umoja hapa inazo alomofu mbili, moja ni /ji/ kama katika ©, na nyingine ni /O/ (kapa) kama katika (a,b). Lakini ni mazingira gani yanatawala utokeaji wa alomofu hizi? Uchunguzi mdogo tu wa maneno mengine ya ngeli hii utaonyesha kuwa maneno yaliyo mengi ni yale ambayo hayaonyeshi alomofu dhahiri ya umoja. Sasa tuseme kuwa alomofu ya msingi ni /O/ (kapa) na kuwa maneno yanayoonyesha /ji/ katika umoja ni vihitilafu ambavyo hatuwezi kuvielezea zaidi? Tunaweza kupata ufafanuzi zaidi wa alomofu hizi kama tukiangalia upatanishi wa maneno ya ngeli hii na maneno ya makundi mengine.
Kuna kanuni moja ya upatanishi kati ya nomino na maneno ya sifa katika Kiswahili ambapo kipatanishi cha sifa kinafanana kiumbo na kiambishi ngeli cha nomino husika. Tuangalie mifano ifuatayo:
a) Chungwa zuri (Machungwa mazuri)b) Bega dogo (Mabega madogo) c) Jiwe kubwa (Mawe makubwa) a) Chungwa jingine (Machungwa mengine) b) Bega jekundu (Mabega mekundu) c) Jiwe jeusi (Mawe meusi) Kutokana na ujuzi wetu wa kanuni za kifonolojia (au tuziite za kimofonolojia kwa vile zinatokea katika uhusiano kati ya mofimu tofauti za lugha, ingawa zinahusu kanuni za fonolojia), tunaweza kuona haraka tofauti kati ya mifano ya (48) na (49). Kanuni inayotawala hapa inaelekea kuwa: alomofu ya umoja ni /O/ ikiwa mzizi wa neno unaanza na konsonanti, na ni /ji/ ikiwa mzizi unaanza na irabu.
Kama tulivyoona katika kanuni za mofimu nyingine, irabu ya kiambishi inadondoshwa au inazawazishwa. Hivyo tunasema kuwa maneno hayo hapo juu yakikatwa katika viambishi na mizizi yataonekana hivi:
a) ji-iwe – jiweb) ji-ingine – j ingine c) ji-ekundu – jekundu d) ji-eusi – jeusi, n.k. (Tunaweza kulinganisha maneno haya na yale ya upatanishi wa ngeli ya kwanza: {mu-ingine – mwingine, mu-ekundu – mwekundu, mu-eusi – mweusi}).
Hapa ni wazi kuwa si rahisi kila mara kuwa na uhakika wa kanuni zinazotawala bila kuwa na uchunguzi wa makini. Mara nyingi inatokea kuwa kuna kanuni maalumu, hata kama zimejificha, na inakuwa lazima kuangalia uhusiano wa maneno katika sentensi, na hivyo kufanya mipaka kati ya mofolojia na sintaksia kuwa finyu sana kama tutakavyoona katika sura inayofuata.
Lakini wakati mwingine, kunakuwa na matatizo ambayo si rahisi kuyapatia uftimbuzi hata kama tutahusisha maneno hayo katika muundo wa sentensi. Kwa mfano, neno linaonekana kuwa lingeweza kuwa na mofinu zaidi ya moja kwa kulihusisha na maneno mengine ya lugha, lakini ukataji wake si dhahiri, kama katika maneno yafuatayo:
a) kaushab) kauka Maneno haya ni vitenzi, na kutokana na viundaji tulivyoangalia, yanaelekea kuwa ni vitenzi-unde, katika mstari mmoja na maneno mengine kama {fupi : fupisha : fupika}. Lakini je, neho-asili lililokuwa msingi wa uundaji ni lipi? Katika Kiswahili hakuna neno *{kau} (sifa) au *{kaua} (kitenzi), ambayo yangeweza kuwa msingi wa maneno haya. Kikazi katika sentensi, hayana tofauti na maneno unde mengine
a) Juma amekausha nguob) Nguo zimekauka. Inawezekana kuwa katika Kiswahili cha zamani kulikuwa na neno ambalo ni msingi wa maneno hayo, lakini hatuwezi kujua lilikuwa lipi. Kuna mifano mingine ya namna hiyo katika Kiswahili. Tukiangalia
a) kana : kanushab) anika : anua Hapa tunaona kuwa kuna mapengo katika sulubu zinazojitokeza. Kwa mfano katika (a) tungetarajia tuwe na neno la Kiswahili {*kanua} kama {funga :fungua}, ambalo ndilo linaoongezewa kiundaji /-sh-/ cha utendesha. Lakini neno hilo halipo kwa wakati huu. Katika (b) matatizo ni kama yale ya maneno ya (52), na si rahisi kueleza jinsi yanavyohusiana katika maumbo yao, ingawa uhusiano wa maana uko wazi.
Katika lugha pia yanaweza kuwepo maneno ambayo yanaonyesha wazi kuwa ni muunganiko wa mofimu-mizizi kadhaa, lakini mizizi hiyo ni ya maneno ambayo hayatumiki tena katika lugha. Kwa mfano neno lifuatalo:
a) mkurugugenziMizizi yote miwili inayounda neno hilo,
b) kuruc) genda ni ya maneno ambayo kwa sasa hayatumiki katika Kiswahili, ingawa kuna ushahidi wa kutosha kuwa kulikuwa na neno {kuru} na {genda} ambayo ndiyo yamebadilika na kuwa maneno ya sasa {kuu} na {enda}. Lakini hiyo ni historia ya neno, na swali bado linabaki, je neno hili katika sarufi ya Kiswahili ya sasa, lifafanuliwe vipi, kama neno-unde, au kama neno-asili, yaani kama {mwanafunzi}, au kama {mtoto}? Hili ni swali ambalo si rahisi kulijibu.
Haya ni machache tu kati ya mambo mengi ambayo yanajadiliwa katika taaluma ya mofolojia. Mengine mengi hatukuyagusia. Lakini ni dhahiri, kutokana na haya machache, kuwa maneno ya lugha ni vipashio tata sana, na kila lugha ina muundo wake tofauti wa maneno. Wakati huo huo tumeona kuwa kuna kanuni ambazo zinaelekea kuwa za jumla zinazohusisha maneno ya lugha moja. Mazoezi yanayofuata yatatoa nafasi ya kuona kanuni tulizojadili zinavyofanya kazi katika lugha tofauti. Na bila shaka utaweza kuongezea mifano mingine kutuka lugha unazozijua. |