MAJINA YA UKOO/NASABA - Printable Version +- JIFUNZE KISWAHILI (https://jifunzekiswahili.co.tz) +-- Forum: My Category (https://jifunzekiswahili.co.tz/forumdisplay.php?fid=1) +--- Forum: Historia ya makabila ya kibantu (https://jifunzekiswahili.co.tz/forumdisplay.php?fid=15) +--- Thread: MAJINA YA UKOO/NASABA (/showthread.php?tid=1561) |
MAJINA YA UKOO/NASABA - MwlMaeda - 11-27-2021 1. Mama/nina: Mzazi wa kike. 2. Baba: Mzazi wa kiume. 3. Kaka: Ndugu wa kiume. 4. Dada: Ndugu wa kike. 5. Nyanya/Bibi: Mama wa baba au mama. 6. Babu: Baba wa mama au baba. 7. Mjukuu: Mtoto wa mwana. 8. Kitukuu: Mwana wa mjukuu. 9. Kilembwe: Mwana wa kitukuu. 10. Kilembwekeza/kining’ina: Mwana wa kilembwe. 11. Ami/amu: Kaka wa baba. 12. Shangazi/mbiomba amati: Dada wa baba. 13. Mjomba/hau: Kaka wa mama. 14. Halati/hale: Dada wa mama bila kubagua kama ndiye mdogo au mkubwa kwa mama yako mzazi. Pia huitwa hale. 15. Mkazahau: Mke wa mjomba. 16. Mkazamwana: Mke wa mwana au mke wa mtoto wako. 17. Mavyaa: Mzazi wa kike wa mume. 18. Bavyaa: Mzazi wa kiume wa mume wako. 19. Mamamkwe: Mama wa mke/Mume. 20. Babamkwe: Baba wa mke/Mume. 21. Mcheja: Mzazi wa mke au mume (mkwe). 22. Kivyere : Jina la wazazi wa mume na wazazi wa mke hutumia kuitana. 23. Mpwa: Mtoto wa dada wa mtu mwanamume; jina analotumia mjomba kumwita mtoto wa dadake. 24. Mkoi: Mtoto wa shangazi, mjomba, halati. 25. Binamu: Mwana wa kiume wa ami. 26. Bintiamu: Mwana wa kike wa ami. 27. Shemeji: Ndugu wa mke au ndugu wa mume. 28. Mama wa kambo: Mama asiyekuzaa lakini anakulea. 29. Baba wa kambo: Baba asiyekuzaa 30. Umbu: Jina waitanalo kaka na dada. Ni jinsi kaka anavyomwita dada naye dada anavyomwita kaka wakiwa wamezaliwa na mzazi mmoja. 31. Ndugu mlungizi: Ndugu anayekufuata 32. Ndugu mlungizi: Ndugu anayekufuata nyuma. 33. Wifi: (a) Mke wa kaka. Iwapo wewe ni msichana, mke wa kaka yako utamwita wifi. (b) Dada wa mume: Iwapo msichana ameolewa dada wa mumewe atamwita wifi. 34. Mwamu/mlamu: a) Kaka wa mke. Mwanamume akioa, kaka wa mkewe atamwita mlamu. b) Mume wa dada: mvulana au mwanamume atamwita mume wa dadaye – mlamu. 35. Mwanyumba: Ni mwanaume mwenzako aliyeoa kutoka boma moja ulikooa wewe. Ni mume wa dada wa mke wako. 36. Mkemwenza/mitara: Jina wanalotumia wanawake walioolewa na mwanamume mmoja. 37. Kifungamimba/ kitindamimba/ mziwanda: Mtoto wa mwisho kuzaliwa katika familia. 38. Mwanambee/kifunguamimba/kichinjamimba: Mtoto wa kwanza kuzaliwa katika familia. 39. Nyanyamkuu: Mama wa nyanya. 40. Babamkuu: Baba wa babu. 41. Maharimu: Mtu usiyeweza kumwoa au kuolewa naye kwa sababu ya uhusiano wa nasaba. 42. Mnuna: Ndugu anayenifuata ndugu mdogo. 43. Baba mkubwa – Ndugu wa kiume, mkubwa wa baba yako. 44. Baba mdogo – Ndugu wa kiume, mdogo wa baba yako. |