Neno Keshokutwa haliunganishwi ni vema kuandika kesho kutwa - Printable Version +- JIFUNZE KISWAHILI (https://jifunzekiswahili.co.tz) +-- Forum: My Category (https://jifunzekiswahili.co.tz/forumdisplay.php?fid=1) +--- Forum: Sarufi na Utumizi wa lugha (https://jifunzekiswahili.co.tz/forumdisplay.php?fid=9) +--- Thread: Neno Keshokutwa haliunganishwi ni vema kuandika kesho kutwa (/showthread.php?tid=1527) |
Neno Keshokutwa haliunganishwi ni vema kuandika kesho kutwa - MwlMaeda - 11-20-2021 MAKOSA yanayojitokeza katika magazeti mengi ya Kiswahili ni kutokana na waandishi kutokuwa makini na wengine kutokuwa na ujuzi wa kutosha katika sarufi na fasihi ya Kiswahili.
Ninaposema waandishi nina maana ya kuwahusisha wataalamu wengine wa uandishi wa habari kama vile wahariri, wahakiki kurasa na wadhibiti maandishi. Hawa wote ni muhimu katika uandishi bora. Hebu soma sentensi zifuatazo :
“Jukwaa la Wanamusanze lina dhumuni la kuhamasisha watu kuchangia sekta za kilimo, siasa, elimu, uchumi, utamaduni na jamii.”
Waandishi wengi huwa hawaelewi kuwa wazungumzaji wanapotumia ‘ma’ mbele ya baadhi ya maneno wanafanya makosa. Kwa mfano liko neno dhumuni ambalo halitumiki kwa usahihi. Kwa usahihi lingekuwa madhumuni ambalo linatumika katika umoja na katika wingi.
Dhumuni haliko katika msamiati wa Kiswahili ila linalazimishwa na wasiokuwa weledi wa lugha hii. Ni sahihi kuandika,
“Jukwaa la Wanamusanze lina madhumuni ya kuhamasisha watu kuchangia sekta ya kilimo, siasa, elimu, uchumi, utamaduni na jamii.”
“Mtizamo wa aina hii ni batili na hauwezi kuleta matunda mazuri.”
Hapa tena kunaandika kama wanavyozungumza watu badala ya kufuata misingi ya uandishi bora. Kuna wakati tunasikia watu wakisema , ‘Mtizamo wangu ni tofauti na wako’.
Hata hivyo, tunapoandika, neno sahihi ni ’Mtazamo’. Hivyo iandikwe,”Mtazamo wa aina hii ni batili na hauwezi kuleta matunda mazuri.”
“Keshokutwa Ijumaa hatma ya madiwani wanane waliotimuliwa itajulikana mjini Kigali”.
Neno keshokutwa haliunganishwi na kuwa neno moja bali ni maneno mawili tofauti. Vilevile tunaandika hatima na wala siyo hatma kama tunavyozungumza.
Hapa tena tunachanganya lugha ya mazungumzo na ile ya kuandika. Kwa hiyo isomeke, “
“ Kesho kutwa Ijumaa hatima ya madiwani wanane waliotumiliwa itajulikana mjini Kigali.”
“Umati wa watu wakifatilia juu ya maiti zilizoingizwa hospitalni hapo.”
Kwa Kiswahili fasaha kuandika “ juu ya” ni makosa. Ilitakiwa kuandikwa kwa kutumia neno “kuhusu’, hivyo isomeke,
“Umati wa watu wakifuatilia kuhusu maiti zilizoingizwa hospitalini hapo.”
|