MyBB Internal: One or more warnings occurred. Please contact your administrator for assistance.

SHAIRI : SIKU YANGU YA KUZALIWA - Printable Version
JIFUNZE KISWAHILI
SHAIRI : SIKU YANGU YA KUZALIWA - Printable Version

+- JIFUNZE KISWAHILI (https://jifunzekiswahili.co.tz)
+-- Forum: My Category (https://jifunzekiswahili.co.tz/forumdisplay.php?fid=1)
+--- Forum: Fasihi simulizi (https://jifunzekiswahili.co.tz/forumdisplay.php?fid=6)
+---- Forum: Ushairi (https://jifunzekiswahili.co.tz/forumdisplay.php?fid=50)
+---- Thread: SHAIRI : SIKU YANGU YA KUZALIWA (/showthread.php?tid=1509)

SHAIRI : SIKU YANGU YA KUZALIWA - MwlMaeda - 11-20-2021

Siku yangu imefika, mimi niliyozaliwa.
Miaka imekatika, kaburi nasogelea.
Mungu wangu kwa hakika, ndivyo livyonipangia.
Tarehe mbili novemba, yangu siku kuzaliwa.

Wenye rika kama langu, hawapo metangulia.
Huu si ujanja wangu, Mola amenipangia.
Itafika zamu yangu, nami tafuata njia.
Tarehe mbili novemba, yangu siku kuzaliwa.

Nawaomba ndugu zangu, makosa mnisamehe.
Hii si dhamira yangu, mabaya niwatendee.
Kwani huu ulimwengu, si makazi ya milele.
Tarehe mbili novemba, yangu siku kuzaliwa.

Nahisi maisha yangu, siku chache mesalia.
Itatoka roho yangu, kuburini kufukiwa.
Nitaacha Mali zangu, hakuna tachochukua.
Tarehe mbili novemba, yangu siku kuzaliwa.

Na hizo amali zangu, zote zilotangulia.
Zitaziba pengo langu, pale nilupokosea.
Ni rudi kwa Mola wangu, ndipo tulupotokea.
Tarehe mbili novemba, yangu siku kuzaliwa.

Sio ndoto asilani, bali ni uhalisia.
Haufiki mara thani, umri nilofikia.
Nimesoma vitabuni, Rasuli katuusia.
Tarehe mbili novemba, yangu siku kuzaliwa.

Mevuka arobaini, lakini si nusu mia.
Namshukuru Manani, hapa nilipofikia.
Nikijafika mwakani, yote kwangu majaliwa.
Tarehe mbili novemba, yangu siku kuzaliwa.

Beti nane ninakoma, mbele sitoendelea.
Ninaomba mwisho mwema, Mola takabali dua.
RamaB ninasimama, kalamu nina achia.

RamaB.
Gongolamboto.
02/11/2019.