SHAIRI: HAKUNA LENYE MWENYEWE - Printable Version +- JIFUNZE KISWAHILI (https://jifunzekiswahili.co.tz) +-- Forum: My Category (https://jifunzekiswahili.co.tz/forumdisplay.php?fid=1) +--- Forum: Fasihi simulizi (https://jifunzekiswahili.co.tz/forumdisplay.php?fid=6) +---- Forum: Ushairi (https://jifunzekiswahili.co.tz/forumdisplay.php?fid=50) +---- Thread: SHAIRI: HAKUNA LENYE MWENYEWE (/showthread.php?tid=1458) |
SHAIRI: HAKUNA LENYE MWENYEWE - MwlMaeda - 11-11-2021 Kuna Mungu na ujuwe, mwajimbo hili sikia, Kiburi kina mwishowe, si mwingine kuyutia, Laweza vunjika jiwe, na nazi ikabakia, Mja hili zingatia, hakuna lenye mwenyewe. Kuna Mungu na ujuwe, usambe sijakwambia, Hakuna lenye mwenyewe, katika hini dunia, Kupaa ashindwe mwewe, aweze pundamilia, Mja hili zingatia, hakuna lenye mwenyewe. Kuna Mungu na ujuwe, kiumbe hebu tulia, Nguvu zisikuzuzuwe, kiburi ukajitia, Simba mbio na mayowe, swala akimuhofia, Mja hili zingatia, hakuna lenye mwenyewe. Kuna Mungu na ujuwe, ndiyo hutuamulia, Anaweza aamuwe, mambo usoyadhania, Sikio kimo kikuwe, cha kichwa kukizidia, Mja hili zingatia, hakuna lenye mwenyewe. 27 February 2018 Jumanne 09:00am Jina la Mtunzi Dotto Rangimoto Jina la Utunzi Jini Kinyonga ☎ +255762845394 Morogoro. |