MyBB Internal: One or more warnings occurred. Please contact your administrator for assistance.

SHAIRI : NZI HAESHI KUFUKUZWA - Printable Version
JIFUNZE KISWAHILI
SHAIRI : NZI HAESHI KUFUKUZWA - Printable Version

+- JIFUNZE KISWAHILI (https://jifunzekiswahili.co.tz)
+-- Forum: My Category (https://jifunzekiswahili.co.tz/forumdisplay.php?fid=1)
+--- Forum: Fasihi simulizi (https://jifunzekiswahili.co.tz/forumdisplay.php?fid=6)
+---- Forum: Ushairi (https://jifunzekiswahili.co.tz/forumdisplay.php?fid=50)
+---- Thread: SHAIRI : NZI HAESHI KUFUKUZWA (/showthread.php?tid=1456)

SHAIRI : NZI HAESHI KUFUKUZWA - MwlMaeda - 11-11-2021

Malenga ngazi za juu, na watunzi chipukizi,
‘nalo swali muda huu, nawaombeni ujuzi,
Yanampata makuu, hapatwi na usingizi,
Nzi heshi kufukuzwa, popote anapokutwa.

Nzi heshi kufukuzwa, nzi hanoye makazi,
Nzi haifai kuuzwa, kifai chake kizazi,
Laiti angecharazwa, na asiwe na makuzi,
Nzi heshi kufukuzwa, popote anapokutwa.

Hafai majalalani, akikutwa akimbizwa,
Akitua dirishani, kutani anabamizwa,
Tena siseme mezani, sikia navyogombezwa,
Nzi heshi kufukuzwa, popote anapokutwa.

Ni kwamba hana makao, ama wa kukataliwa,
Wapo wengi warukao, hifadhi wanapatiwa,
Nzi hatakwi uchao, maliwato atolewa,
Nzi heshi kufukuzwa, popote anapokutwa.

Tano naweka utuo, siwezi kuendelea,
Naiona mizabuo, Nzi inamkolea,
Mje na mchanganuo, majibu kuniletea,
Nzi heshi kufukuzwa, popote anapokutwa.

©Mary Marcus,
Mbezi Louis,
04.12.2019. 1:45PM
Dar es Salaam
Email: marymarcusg@gmail.com