SHAIRI: NIMEMKUMBUKA MAMA - Printable Version +- JIFUNZE KISWAHILI (https://jifunzekiswahili.co.tz) +-- Forum: My Category (https://jifunzekiswahili.co.tz/forumdisplay.php?fid=1) +--- Forum: Fasihi simulizi (https://jifunzekiswahili.co.tz/forumdisplay.php?fid=6) +---- Forum: Ushairi (https://jifunzekiswahili.co.tz/forumdisplay.php?fid=50) +---- Thread: SHAIRI: NIMEMKUMBUKA MAMA (/showthread.php?tid=1411) |
SHAIRI: NIMEMKUMBUKA MAMA - MwlMaeda - 11-02-2021 NIMEMKUMBUKA MAMA Ingelikua hiari, 'pite hapa nende kule, Wala nisingesubiri, niambiwe nenda mbele, ningepita sirisiri, hadi ningefika pale, Nimuone mama yangu. Ama niseme usiku, huamka watu wale, ningekesha kila siku, nimuone mama yule, niende huko na huku, nimpigie kelele, Lakini hawaamki. Amelala mama yangu, usingizi wa milele, hauniishi uchungu, ati nitulie nile, afua hii wenzangu, siipati tangu pale, Mama aliponiacha. Kinauma kitu hiki, heri niumwe upele, nalia sitamaniki, ninapungua umbile, kunyamazishwa sitaki, nacheni mie nilile, hamjui paumavyo. Ni yasemayo ya kweli, sidhani ya Mzingile, Yanitesa hii hali, yanifanya nisilale, hata upikwe ugali, na mboga ya matembele, Simsahau mamangu. Jamani olele mama, nalia olelelele, mamangu umenihama, umetangulia kule, kuniacha mie ndama, nitange huko na kule, Ungerudi mama yangu. Nandike nini kingine, mama pumzika pale, sipate tabu nyingine, Kama wakosefu wale, siku moja tukutane, mahala ahera kule, Baibai mama yangu. Mtunzi Filieda Sanga Mama B Mabibo Dsm 0753738704 |