SHAIRI: KAZI YA NANI MALEZI? - Printable Version +- JIFUNZE KISWAHILI (https://jifunzekiswahili.co.tz) +-- Forum: My Category (https://jifunzekiswahili.co.tz/forumdisplay.php?fid=1) +--- Forum: Fasihi simulizi (https://jifunzekiswahili.co.tz/forumdisplay.php?fid=6) +---- Forum: Ushairi (https://jifunzekiswahili.co.tz/forumdisplay.php?fid=50) +---- Thread: SHAIRI: KAZI YA NANI MALEZI? (/showthread.php?tid=1329) |
SHAIRI: KAZI YA NANI MALEZI? - MwlMaeda - 10-19-2021 KAZI YA NANI MALEZI? Baba: Baba nipo kataani, sikubali jambo hili, Hanifiki akilini, kwani sioni halali, Mtoto alee nani, baba! Hilo sikubali, Kazi ya mama malezi, baba natafuta mali. Mama: Bwana ungebadilika, zetu enzi sio zile, Tena ufanye haraka, utaaibika mbele, hicho unachotamka, nakucheka ni ukale, Zimebadilika zama, malezi mama na baba. Baba: Shule imekuharibu, mwanamke kaa chini, Umeishiwa adabu, hiyo ni tabia gani? Mie na zangu sharubu, huyo mwana tampani? Kazi ya mama malezi, baba natafuta mali. Mama: Ishushe yako sauti, taamsha majirani, Ukujalie umati, katikati ya manani, Wanitupia kijiti, nilee peke kwa nini, Zimebadilika zama, malezi mama na baba. Baba: Umeanza mazoea, kielimu uchopata, Ujue nakushangaa, mama uache Matata, Nani unamtupia, hiyo kazi ulopata? Kazi ya mama malezi, baba natafuta mali. Mama: Wajua kazi malezi, au bure unafoka? Kikwachia hauwezi, majasho yatakutoka, Tofauti chini weka, tufanye sote malezi, Zimebadilika zama, malezi mama na baba. Baba: Hebu tia umuhimu, hicho witacho malezi, Bure unanilaumu, ninaona ni upuzi, Hakinipi utimamu, wawili kwa moja kazi, Kazi ya mama malezi, baba natafuta mali. |