SHAIRI: HAIKUWA NIA YANGU - Printable Version +- JIFUNZE KISWAHILI (https://jifunzekiswahili.co.tz) +-- Forum: My Category (https://jifunzekiswahili.co.tz/forumdisplay.php?fid=1) +--- Forum: Fasihi simulizi (https://jifunzekiswahili.co.tz/forumdisplay.php?fid=6) +---- Forum: Ushairi (https://jifunzekiswahili.co.tz/forumdisplay.php?fid=50) +---- Thread: SHAIRI: HAIKUWA NIA YANGU (/showthread.php?tid=1321) |
SHAIRI: HAIKUWA NIA YANGU - MwlMaeda - 10-17-2021 HAIKUWA NIA YANGU Utenzi naambiliza, Kwakowe Mola muweza, Waja kinisikiliza, Tanipatia afua. Afua tanipatia, Moyo upate kutua, Machungu yamenipea, Bado roho kuzimia. Niwambie kisa hiki, Wanijue alaiki, Ya kuwa chanzo ni dhiki, Tabu kuniangukia. Madhara yamenimea, Kila siku yanakua, Ndugu na wazazi pia, Lawama kunitumia. Lawama kunitumia, Jina bovu niambia, Leo wazi tawambia, Akili kuwafunua. Shule ilikuwa mbali, Ilipo nyumba mahali, Naanza kutawakali, Masikio nipatia. Nilizichoka adhabu, Walimu kunipa tabu, Na maneno ya aibu, Haweshi kuniambia. Alitokea kijana, Wa makamu sio sana, Kaniomba msichana, Pikipiki kuikwea. Ilikuwa siku zote, Nendapo nirudi sote, Mara ikawa popote, Tukajenga mazoea. Pia kinipa zawadi, Kupokea Sina budi, Kumbe yako makusudi, Kijana kunongopea. Siku moja katikati, Msituni kwenye miti, Kijana lijidhatiti, Mimba akanipatia. Hali nami si mwerevu, Ngawa mie msikivu, Ujinga ni ulemavu, Madhara sikuyajua. Ndipo lianza kutuna, Langu tumbo kuwa pana, Nanenepa ndiyo Mana, Moyoni kujiwazia. Mashaka yaliwangia, Walimu Wazazi pia, Umri sijatimia, Kuleta mwana mng'aa. Vipimo vilishangaza, Shule nikaipoteza, Yangu mimba kuikuza, Hadi leo nimezaa. Natoa yangu maoni, Tujengeeni mabweni, Kutiwa majaribuni, Itakomea tabia. Na mtupe shahiki, Daftari nazo biki, Inaturubuni dhini, Wazazi nawaambia. Elimu tupatieni, Kuwa mimba kitu gani, Hivyo tuipate lini, Ni elimu ya jinsia. Adhabu sio kipimo, Tabia kuja kikomo, Bure mtapiga domo, Kudhani mnatulea. Kudhani mnatulea, Nalipinga kusikia, Malezi mwapuuzia, Mnadai mwatulea. Siendelezi shairi, Sije niona jeuri, Nimewapa hiyo Siri, Vipi mimba hutokea. Mtunzi Filieda Sanga Mama B Mabibo Dsm 0753738704 |