SHAIRI: TUNZA UNACHOMILIKI - Printable Version +- JIFUNZE KISWAHILI (https://jifunzekiswahili.co.tz) +-- Forum: My Category (https://jifunzekiswahili.co.tz/forumdisplay.php?fid=1) +--- Forum: Fasihi simulizi (https://jifunzekiswahili.co.tz/forumdisplay.php?fid=6) +---- Forum: Ushairi (https://jifunzekiswahili.co.tz/forumdisplay.php?fid=50) +---- Thread: SHAIRI: TUNZA UNACHOMILIKI (/showthread.php?tid=1319) |
SHAIRI: TUNZA UNACHOMILIKI - MwlMaeda - 10-15-2021 TUNZA UNACHOMILIKI Tunza unachomiliki, mwezenu nawaambia, Usikijazie dhiki, moyoni kikaumia, Kitunze pasi na chuki, mapenzi yakakolea, Tunza unachomiliki, huba lisije regea. Tunza unachomiliki, yawe yako mazoea, Kitunze kinacho haki, sikifanyie sagua, Kijibu pasi hamaki, kisijione bandia, Tunza unachomiliki , kisije kutaataa. Tunza unachomiliki, mlo ukakipatia, Kipikie hata keki, tumboni kikaitia, Nacho kikawe mithaki, mate ukakimezea, Tunza unachomiliki, ngozi isije chanika. Tunza unachomiliki, mema ukaamania, Sije itwa baramaki, jina ninalochukia, Kutunza ukadiriki, weye ukajikomboa, Tunza unachomiliki, kutunza siyo hatia. Beti sita hazifiki, wa tano ninakomea, Niiweke yangu maki,hapo nije kuanzia, Tunza siwe mtaliki, ufe hujajizalia, Tunza unachomiliki, nadama hitokujia. Mwalimu Nyakundi Malenga Tembo mla nyama Shule ya upili ya Amabuko, Keroka. 11. 10. 2021. ? |