Sifa mhimu anazotakiwa kuwa nazo msomaji yoyote wa lugha - Printable Version +- JIFUNZE KISWAHILI (https://jifunzekiswahili.co.tz) +-- Forum: My Category (https://jifunzekiswahili.co.tz/forumdisplay.php?fid=1) +--- Forum: Chuo (https://jifunzekiswahili.co.tz/forumdisplay.php?fid=3) +---- Forum: Shahada (https://jifunzekiswahili.co.tz/forumdisplay.php?fid=20) +----- Forum: Maswali na majibu (https://jifunzekiswahili.co.tz/forumdisplay.php?fid=24) +----- Thread: Sifa mhimu anazotakiwa kuwa nazo msomaji yoyote wa lugha (/showthread.php?tid=1300) |
Sifa mhimu anazotakiwa kuwa nazo msomaji yoyote wa lugha - MwlMaeda - 10-06-2021 Misingi katika kusoma Kusoma ni nini? Kusoma kunaelezwa katika ngazi nne (i) uwezo wa kutambua maandishi katika maumbo yake mbalimbali kwa kuyahusisha maumbo hayo na kitu, jambo au tendo. (ii) Uwezo wa kuyakabili maandishi kwa kasi na wepesi bila kupoteza kiini chake. (iii) Uwezo wa kuelewa maana iliyomo bila vipingamizi. (iv) Uwezo wa kuyahusisha maandishi na uzoefu wake wa kila siku. (v) Uwezo wa kuzingatia na kuyatumia yale yote yaliyo muhimu na kuyafanya sehemu ya maisha. kwa kifupi kusoma ni ufumbuzi wa maandishi anaofanya msomaji. Katika mawasiliano maandishi (fumbo) – kusoma ni mawasiliano na kikomo ni macho (mapokeo), utambuzi, tafsiri, maana, uzingatiaji kumbukumbu na kadhalika wa msomaji. |