SHAIRI: HONGERA MWALIMU - Printable Version +- JIFUNZE KISWAHILI (https://jifunzekiswahili.co.tz) +-- Forum: My Category (https://jifunzekiswahili.co.tz/forumdisplay.php?fid=1) +--- Forum: Fasihi simulizi (https://jifunzekiswahili.co.tz/forumdisplay.php?fid=6) +---- Forum: Ushairi (https://jifunzekiswahili.co.tz/forumdisplay.php?fid=50) +---- Thread: SHAIRI: HONGERA MWALIMU (/showthread.php?tid=1299) |
SHAIRI: HONGERA MWALIMU - John John - 10-05-2021 HONGERA MWALIMU Nimeishika kalamu, ya moyoni kuongea, Uyasikie mwalimu, kila kona ya dunia, Wewe ni mtu muhimu, nani asiyelijua? Hongera sana mwalimu, Rahmani akujalie. Fani yako ni adhimu, werevu wanatambua, Kuandaa watalamu, tena waliobobea, Endeleza gurudumu, maarifa kuyatoa, Hongera sana mwalimu, Rahmani akujalie. Ninamuomba Manani, akujalie afia, Akutoe dhorubani, uishi 'kifurahia, Daima takuthamini, jahara nakuambia, Hongera sana mwalimu, Rahmani akujalie. Nibu naishusha chini, tamati nimefikia, Yaliyokuwa moyoni, tayari nimeyatoa, Namshukuru Manani, kipaji kunijalia, Hongera mwalimu, akujalie Rahmani. ********************************************** Mtunzi: JOHN LUKAS JOHN Mwanafunzi, Chuo Kikuu Mzumbe 0788514751/0747225775 jjohnlukas0788@gmail.com |