MyBB Internal: One or more warnings occurred. Please contact your administrator for assistance.

Tofauti ya irabu za Kiswahili na irabu za Kiingereza - Printable Version
JIFUNZE KISWAHILI
Tofauti ya irabu za Kiswahili na irabu za Kiingereza - Printable Version

+- JIFUNZE KISWAHILI (https://jifunzekiswahili.co.tz)
+-- Forum: My Category (https://jifunzekiswahili.co.tz/forumdisplay.php?fid=1)
+--- Forum: Chuo (https://jifunzekiswahili.co.tz/forumdisplay.php?fid=3)
+---- Forum: Shahada (https://jifunzekiswahili.co.tz/forumdisplay.php?fid=20)
+----- Forum: Maswali na majibu (https://jifunzekiswahili.co.tz/forumdisplay.php?fid=24)
+----- Thread: Tofauti ya irabu za Kiswahili na irabu za Kiingereza (/showthread.php?tid=1292)

Tofauti ya irabu za Kiswahili na irabu za Kiingereza - MwlMaeda - 10-02-2021

Ni tofauti zipi zilizopo kati ya fonimu irabu za Kiswahili na fonimu irabu za Kiingereza?
MAJIBU
Irabu ni aina ya sauti ya lugha inayotamkwa bila kuwapo na kizuizi chochote kwenye mkondo wa hewa kutoka mapafuni kupitia kinywani na puani.
Irabu za Kiswahili na zile za Kiingereza hutofautiana katika vipengele anuai kama ifuatavyo.
·Kiswahili kina irabu tano wakati Kiingereza kina irabu 20
·Kiswahili hakina irabu za kati lakini Kiingereza kina irabu za kati
·Kiswahili hakina mwambatano wa irabu mbili kwa moja lakini Kiingereza kina mwambatano wa irabu mbili kwa moja
·Katika Kiswahili irabu haiwezi kusimama peke yake lakini kwenye Kiingereza irabu huweza kusimama peke yake mf. A man
·Katika Kiswahili irabu haziwezi kutokea zaidi ya mbili zikifuatana lakini katika Kiingereza huweza kutokea mf. Lawyer /lɔia/, buyer /baia/

RE: Tofauti ya irabu za Kiswahili na irabu za Kiingereza - MwlMlela - 10-02-2021

Somo zuri sana, nashauri wataalamu wengine wa isimu waongezee mifano