SHAIRI: MAMA WA NYUMBANI - Printable Version +- JIFUNZE KISWAHILI (https://jifunzekiswahili.co.tz) +-- Forum: My Category (https://jifunzekiswahili.co.tz/forumdisplay.php?fid=1) +--- Forum: Fasihi simulizi (https://jifunzekiswahili.co.tz/forumdisplay.php?fid=6) +---- Forum: Ushairi (https://jifunzekiswahili.co.tz/forumdisplay.php?fid=50) +---- Thread: SHAIRI: MAMA WA NYUMBANI (/showthread.php?tid=1281) |
SHAIRI: MAMA WA NYUMBANI - MwlMaeda - 09-27-2021 MAMA WA NYUMBANI Cheo hiki sikitaki, Kuwa mama wa nyumbani, Tena nasema sitaki, Kaumu sikilizeni, Eti chini sijiweki, Kutwa nipo sumbukoni, Sitaki! Cheo kisicho heshima, Wenzangu wananihizi, Ndio Mana nalalama, Nafasi hii kuhozi, Na Sasa kazi naigoma, Kufanya tena siwezi, Sitaki! Kazi isiyo malipo, Hainipi afueni, Ningeokota makopo, Nondoke umasikini, Hivi Sasa niponipo, Mafaufu magauni, Sitaki! Nipike nioshe vyombo, Kisha nguo nizifue, Wala siishiwi mambo, Eti sema nipumue, Kazi napiga kikumbo, Nyingine nijifanyie, Sitaki! Wakirudi makazini, Hawana adabu katu, Hujiona wathamani, Nami wanione fyatu, Wasemavyo Nina nini, Jamani huo ndo utu? Sitaki! Maisha yangu ni duni, Zangu shida haziishi, Mie nakosa sabuni, Mavazi pia marashi, Kucha kutwa sumbukoni, Hivi kazi hazinishi, Sitaki! Shairi ninalifunga, Mie mama wa nyumbani, Safari ninaipanga, Kubadilisha sidhani, Mechoka kutangatanga, Hizi kazi za nyumbani, Sitaki! Mtunzi Filieda Sanga Mama B Mabibo Dsm 0753738704 |