SHAIRI: IMEMNAMBA DUNIA - Printable Version +- JIFUNZE KISWAHILI (https://jifunzekiswahili.co.tz) +-- Forum: My Category (https://jifunzekiswahili.co.tz/forumdisplay.php?fid=1) +--- Forum: Fasihi simulizi (https://jifunzekiswahili.co.tz/forumdisplay.php?fid=6) +---- Forum: Ushairi (https://jifunzekiswahili.co.tz/forumdisplay.php?fid=50) +---- Thread: SHAIRI: IMEMNAMBA DUNIA (/showthread.php?tid=1269) |
SHAIRI: IMEMNAMBA DUNIA - MwlMaeda - 09-24-2021 IMEMNAMBA DUNIA 21-09-2021 Kajitanua kifua, akatembea kwa ndaro Mabega kuyanyanyua, asijitiye kasoro Fahamu akajitoa, kwa watu kufanya kero Azolewa kwa pauro, imemnamba dunia. Imemnamba Dunia, muache agaregare Mambo yamemfikia, acha roho yampare Yale aliyoringia, sasa acha yamkere Sasa aliwa ni chore, imemnamba dunia. Imemnamba Dunia, kichwani sasa hanani Mambo aliyavamia, kuyaweka kifuani Sasa yamning'inia, hakika yu taabani Hanani sasa hanani, imemnamba dunia. Imemnamba Dunia, yamfundisha adabu Wa vyele hakusikia, na hii ndio sababu Njiani akapotea, jua likamsulubu Sasa amekuwa bubu, imemnamba dunia. Imemnamba Dunia, muacheni atuliye Hakika kajichokea, kiasi ajililiye Majuto ajijutia, acha leo aumiye Akomeshwe akomaye, imemnamba dunia. Ali Ben Othman Zanzibar 2:12 21/9/2021 |