NYIMBO ZA KIZALENDO - Printable Version +- JIFUNZE KISWAHILI (https://jifunzekiswahili.co.tz) +-- Forum: My Category (https://jifunzekiswahili.co.tz/forumdisplay.php?fid=1) +--- Forum: Fasihi simulizi (https://jifunzekiswahili.co.tz/forumdisplay.php?fid=6) +---- Forum: Ushairi (https://jifunzekiswahili.co.tz/forumdisplay.php?fid=50) +---- Thread: NYIMBO ZA KIZALENDO (/showthread.php?tid=1221) |
NYIMBO ZA KIZALENDO - MwlMaeda - 09-10-2021 TANZANIA TANZANIA NAKUPENDA Tanzania Tanzania, nakupenda kwa moyo wote Nchi yangu Tanzania, jina lako ni tamu sana Nilalapo nakuota wewe, niamkapo ni heri mama wee Tanzania Tanzania nakupenda kwa moyo wote. Tanzania Tanzania , ninapokwenda safarini Kutazama maajabu, biashara nayo makazi Sitaweza kusahau mimi mambo mema ya kwetu kabisa Tanzania Tanzania nakupenda kwa moyo wote Tanzania Tanzania karibu wasio kwao Kwenye shida na taabu kukimbizwa na walowezi Tanzania yawakaribisha tuungane kiume chema wee Tanzania Tanzania nakupenda kwa moyo wote Tanzania Tanzania watu wako ni mema sana Nchi nyingi zakuota nuru yako hakuna tena Na wageni wakukimbilia ngome yako imara kweli wee Tanzania Tanzania mola awe nawe daima TAZAMA RAMANI Tazama ramani utaona nchi nzuri Yenye mito na mabonde mengi ya nafaka, Nasema kwa kinywa halafu kwa kufikiri, Nchi hiyo mashuhuri huitwa Tanzaniaaaaaaaaaa…. Majira yetu haya, yangekuwaje sasa Utumwa wa nchi, Nyerere ameukomesha X2 Chemchem ya furaha amani nipe tumaini, Kila mara niwe kwako nikiburudika, Nakupenda sana hata nikakusitiri, Nitalalamika kukuacha Tanzania. Majira yetu haya, yangekuwaje sasa Utumwa wa nchi, Nyerere ameukomesha X2 Nchi yenye azimio lenye tumaini, Ndiwe peke yako mwanga wa Watanzania, Ninakuthamini hadharani na moyoni, Unilinde name nikulinde hata kufa. Majira yetu haya, yangekuwaje sasa Utumwa wa nchi, Nyerere ameukomesha X2 RE: NYIMBO ZA KIZALENDO - John John - 09-11-2021 Safi sana kwa kutukumbusha |