SHAIRI: CHAJA - Printable Version +- JIFUNZE KISWAHILI (https://jifunzekiswahili.co.tz) +-- Forum: My Category (https://jifunzekiswahili.co.tz/forumdisplay.php?fid=1) +--- Forum: Fasihi simulizi (https://jifunzekiswahili.co.tz/forumdisplay.php?fid=6) +---- Forum: Ushairi (https://jifunzekiswahili.co.tz/forumdisplay.php?fid=50) +---- Thread: SHAIRI: CHAJA (/showthread.php?tid=1138) |
SHAIRI: CHAJA - MwlMaeda - 09-04-2021 CHAJA Natanguliza salamu,pate juwa hali zenu Muwazima ndani humu,nijuzeni mi mwenzenu Nimekuja na nudhumu,tegesheni ndewe zenu Kubadili simu chaja,mwaharibu simu zenu Kina dada kina mama,niwenu uno ujumbe Moja chaja ni salama,nisikia we kiumbe Epuka kuhamahama,ruka ruka kumbekumbe Kubadili simu chaja,mwaharibu simu zenu Chaja huwa tofauti,zipo ndefu zipo fupi Zipo za kati kwa kati,chagua wataka ipi Zipo nyeusi tititi,samawati na nyeupi Kubadili simu chaja,mwaharibu simu zenu Simuyo waiumiza,yapanuka kichajio Yashindwa moto ingiza,unakosa mtandao Unabaki kwenye giza,huna tena kimbilio Kubadili simu chaja,mwaharibu simu zenu Mkono nawapungia,bai bai kwa herini Tano beti napumua,muhimu zingatieni Msije mbele jutia,tukawakosa hewani Kubadili simu chaja,mwaharibu simu zenu. Chotara Mswahili *Cm*⚓? RE: SHAIRI: CHAJA - John John - 09-05-2021 (09-04-2021, 08:57 PM)MwlMaeda Wrote: CHAJA Shairi zuri, ujumbe mzuri. Kongole kwa mtunzi. Kubadili simu chaja, mwaharibu simu zenu |