MyBB Internal: One or more warnings occurred. Please contact your administrator for assistance.

OSW 123/133: FASIHI YA KISWAHILI NADHARIA NA UHAKIKI - Printable Version
JIFUNZE KISWAHILI
OSW 123/133: FASIHI YA KISWAHILI NADHARIA NA UHAKIKI - Printable Version

+- JIFUNZE KISWAHILI (https://jifunzekiswahili.co.tz)
+-- Forum: My Category (https://jifunzekiswahili.co.tz/forumdisplay.php?fid=1)
+--- Forum: Chuo (https://jifunzekiswahili.co.tz/forumdisplay.php?fid=3)
+---- Forum: Shahada (https://jifunzekiswahili.co.tz/forumdisplay.php?fid=20)
+----- Forum: Maswali na majibu (https://jifunzekiswahili.co.tz/forumdisplay.php?fid=24)
+----- Thread: OSW 123/133: FASIHI YA KISWAHILI NADHARIA NA UHAKIKI (/showthread.php?tid=1095)

OSW 123/133: FASIHI YA KISWAHILI NADHARIA NA UHAKIKI - MwlMaeda - 09-01-2021

SWALI: Fasihi ya jamii yako ndogo ina nafasi gani katika kuimarisha na kuendeleza fasihi ya kitanzania kwa lugha ya Kiswahili?
JIBU
Fasihi ya kitanzania  kwa lugha ya Kiswahili ni matokeo ya mchango wa fasihi za jamii ndogondogo zilizokusanywa pamoja kwa kutumia lugha ya Kiswahili kama kielelezo cha utamaduni wa jamii ya watanzania kwa ujumla.
Mchango wa fasihi ya jamii ndogo unajidhihirisha katika fasihi ya kitanzania kwa lugha ya Kiswahili kama ifuatavyo:
Ngoma, ngoma ni moja ya vipengele vya fasihi kwa Kiswahili ambavyo hutoka katika fasihi ya jamii ndogondogo kwa mfano ngoma ya jamii ya wamakonde (sindimba), ngoma ya Wazaramo (mdundiko), zimechangia kuwepo kwa utanzu wa ngoma katika fasihi ya kitanzania iliyoandaliwa kwa lugha ya Kiswahili.
Matambiko, ni fasihi ya jamii ndogo ndogo na kila jamii huwa na kaida zake na mahali maalumu pa kutendea. Kipengele hiki kinapochambuliwa na kujadiliwa katika fasihi kwa lugha ya Kiswahili hakiondolewi asili yake wala hakifanywi kuwa kipengele cha jumla kwa jamii zote.
Hadithi, masimulizi ya kihadithi katika fasihi kwa Kiswahili hutoka kwenye masimulizi ya jamii ndogo ndogo zilizopitia matukio mbalimbali yaliyoacha kumbukumbu zenye masimulizi hayo kwa mfano jamii ya Wahehe inatoa masimulizi ya Mkwawa, jamii ya Wasukuma inatupa masimulizi ya mtu ajulikanaye kama Ng’wanamalundi lakini pia jamii ya Wangozi inatupa masimulizi ya Fumo Liyongo. Kwa hiyo masimulizi ya kihadithi katika fasihi kwa lugha ya Kiswahili ni mchango toka fasihi za jamii ndogo.
Elimu ya jadi, itolewayo kwa vijana wa kike kama unyago na wa kiume kupitia jando ni mchango wa fasihi za jamii zenye kutenda mambo hayo, hivyo fasihi ya kitanzania kwa lugha ya Kiswahili inaposhughulikiwa katika kuchambua masuala ya jando na unyago ni kwa sababu masuala hayo yapo ndani ya jamii zinazounganishwa kupitia fasihi kwa lugha ya Kiswahili
Umoja na mshikamano, katika jamii huimarika na matabaka huondoka pale jamii inaposhirikiana katika matukio ya furaha au huzuni kwa mfano katika sherehe mbalimbali zenye kukusanya watu wa jamii tofauti si ajabu kuchezwa ngoma yenye asili ya jamii mojawapo kati ya jamii zilizokusanyika, mathalani ngoma ya jamii ya Kichaga huweza kuchezwa hata na watu wasio Wachaga na kufanya ngoma hiyo kuwa ya wote.
Mwingiliano wa kijamii, kwamba fasihi kwa lugha ya Kiswahili inasababisha mila na desturi za jamii ndogondogo kuonekana kama kitu kimoja na kuchochea mwingiliano wa jamii hizo hata kufikia hatua ya kuoana watu wa jamii tofauti kwa kuzingatia utaratibu wa mila na desturi zilizorekebishwa hata kupunguza athari zilizokuwepo mwanzo.
Maendeleo na kuimarika kwa fasihi ya kitanzania kwa lugha ya Kiswahili ni matokeo ya mchango mkubwa toka fasihi za jamii ndogondogo zilizojitoa katika upekee na kuleta ujumla wa kifasihi.