MyBB Internal: One or more warnings occurred. Please contact your administrator for assistance.

MASWALI NA MAJIBU – 9: DARASA LA 3 & 4 - Printable Version
|
MASWALI NA MAJIBU – 9: DARASA LA 3 & 4 - Printable Version
+- JIFUNZE KISWAHILI (https://jifunzekiswahili.co.tz)
+-- Forum: My Category (https://jifunzekiswahili.co.tz/forumdisplay.php?fid=1)
+--- Forum: Shule ya Msingi (https://jifunzekiswahili.co.tz/forumdisplay.php?fid=62)
+---- Forum: Maswali na majibu (https://jifunzekiswahili.co.tz/forumdisplay.php?fid=65)
+---- Thread: MASWALI NA MAJIBU – 9: DARASA LA 3 & 4 (/showthread.php?tid=1070)
|
MASWALI NA MAJIBU – 9: DARASA LA 3 & 4 - MwlMaeda - 08-30-2021
MASWALI NA MAJIBU – 9: DARASA LA 3 & 4
SEHEMU A: Pigia mstari neno tofauti
- Dada, mama, babu, shangazi
- Cheza, imba, inama, matunda
- Mia, tisini, kumi, namba
- Dereva, fundi, kipofu, mvuvi
- Samba, chui, kondoo, ndovu
SEHEMU B:
- Mbwa wetu akimwona adui…………….
(a) hulia (b) huruka © hubweka (d) hucheza
- ……………….maji ya kunywa ili yawe salama
(a) chuja (b) chemsha © poza (d) koroga
- Waliposafiri waliona nyumba nyingi………ya barabara.
(a) juu (b) chini © nje (d) kando
- Mtoto wa mwisho kuzaliwa huitwa…………mimba.
(a) kifungua (b) kianza © kitinda (d) mwisho
- Fundi seremala ametengeneza…………….
(a) thamani (b) sanani © samani (d) samanini
SEHEMU C: Methali, nahau, vitendawili na misemo
- Tamaa mbele mauti……………
(a) kati (b) kidogo © nyuma (d) mbele
- Mariam ana mkono wa birika. Neno lililopigiwa mstari maana yake ni.
(a) mwizi (b) mlevi © mtukufu (d) mchoyo
- Leo ni leo asemaye kesho ni……………..
(a) mjanja (b) mkweli © mjinga (d) mwongo
- Mama hachoki kunibeba. Tegua kitendawili…………..
(a) kiti (b) meza © kitanda (d) punda
- Teketeke huzaa gumugumuna gumugumu huzaa teketeke. Tegua kitendawili.
(a) papai (b) mhindi © ndizi (d) nanasi
SEHEMU D:
- Wingi wa neno saa ni…………………
(a) saa (b) masaa © misaa (d) lisaa
- Kinyume cha neno anza ni …………….
(a) mianzo (b) maliza © anzisha (d) anzia
- Juma ni mjanja kama…………………………
(a) fisi (b) nguruwe © sungura (d) tembo
- Bwana afya ………………kuzingatia kanuni bora za afya.
(a) alitusamehe (b) alitukanya © alitukaripia (d) alituhimiza
- Ali …………..usingizini baada ya mbu kumshambulia.
(a) jigambo (b) jitapa © jipa moyo (d) zinduka
SEHEMU E: UFAHAMU
Familia yam zee Bulicheka ina watoto sita. Watoto wawili wakikeni Rabia na Riziki. Watoto wawili wa kiume ni Joseph na Joakim. Mtoto wa kwanza kuzaliwa ni Roziana. Kitinda mimba ni Joakim. Riziki ni mtoto wa pili kuzaliwa. Watoto wote wa mzee Bulicheka wamesoma hadi chuo kikuu. Kila mmoja ana kazi yake. Joakim ni rubani. Riziki ni muuguzi. Watoto wengine ni walimu.
MASWALI
- Kifungua mimba katika familia yam zee Bulicheka ni nani?
(a) Joseph (b) Riziki © Roziana (d) Joakim
- Joakim ni mtoto wa ngapi?
(a) wa mwisho (b) wawili © watatu (d) wa nne
- Watoto wangapi wa mzee Bulicheka hawakutajwa?
(a) wa kwanza (b) wawili © watatu (d) wanne
- Nani kati yao anafanya kazi hospitalini?
(a) Joakim (b) Roziana © Riziki (d) Joseph
- Riziki ni mtoto wa ngapi kuzaliwa?
(a) wa kwanza (b) wa pili © wa tatu (d) wa nne
MAJIBU
- Babu
- Matunda
- Namba
- Kipofu
- Kondoo
- C
- B
- D
- C
- C
- C
- D
- D
- C
- B
- A
- B
- C
- D
- D
- C
- A
- B
- C
- B
|