SHAIRI: NAWAENZI MAGALACHA - Printable Version +- JIFUNZE KISWAHILI (https://jifunzekiswahili.co.tz) +-- Forum: My Category (https://jifunzekiswahili.co.tz/forumdisplay.php?fid=1) +--- Forum: Fasihi simulizi (https://jifunzekiswahili.co.tz/forumdisplay.php?fid=6) +---- Forum: Ushairi (https://jifunzekiswahili.co.tz/forumdisplay.php?fid=50) +---- Thread: SHAIRI: NAWAENZI MAGALACHA (/showthread.php?tid=1062) |
SHAIRI: NAWAENZI MAGALACHA - MwlMaeda - 08-29-2021 NAWAENZI MAGALACHA Kuna wale waasisi, walotunga tungo hizi, Hao litufunza sisi, Leo tuitwe wajuzi, Zao kazi si nyepesi, kweli walifanya kazi, Na kama sio Shaban, Sanga ningetunga nini? Mfano yule Abedi, aloandika Sheria, Nasi tusizikaidi, tuzifate kwa hatua, Hapo twatia juhudi, upeoni tukapea, Na kama sio Abedi, Sanga ningetoka wapi? Mathias Mnyampala, kwa tungo hizi mjuzi, Kutunga bila kulala, beti mashazi mashazi, Bila huyu mie wala, nani angenimaizi, Matunda ya Mnyampala, Sanga ni nambari wani. Mithili ya Mulokozi, yule bwana maridadi, Ameziandika kazi, siziwezi kwa idadi, Hakika huyu mjuzi, hutunga kwa makusudi, Bila Bwana Mulokozi, Sanga angeota wapi? Kahigi Kulikoyela, kwa kazi hizi mweledi, Hupangilia muwala, kweli amejitahidi, Kwake kutunga ni mila, hakufanya ukaidi, Kama sio mtu huyu, nami nisingekuwapo. Namkumbuka Kandoro, mtunzi kule zamani, Alipanga mishororo, yenye vina na mizani, Tena haina kasoro, kweli nawaambieni, Kandoro naye sawia, amenikuza mtunzi. Naye Sudi Andanenga, mkali wa tungo hizi, Bahari alizitunga, mtunzi nizibarizi, Sheria alizichunga, na kutunga hatelezi, Ai Sudi Andanenga, bila huyo ni udhia. Mwamkumbuka Mloka, yule Charles mwamjua, Hapa ninamtamka, naye amenipa njia, Zake mbinu nimeshika, naanza kuzitumia, Hao baadhi watunzi, niwatao magalacha. Kadi tamati nafunga, siendelezi shairi, Beti nilizozipanga, nanyi Sasa mtakiri, Kuwa tunalvipanga, walotunga Mashairi, Ndio maana mie Sanga,kutunga Wala sikomi. Mtunzi Filieda Sanga Mama B Mabibo Dsm 0753738704 |