SHAIRI: MAMA - Printable Version +- JIFUNZE KISWAHILI (https://jifunzekiswahili.co.tz) +-- Forum: My Category (https://jifunzekiswahili.co.tz/forumdisplay.php?fid=1) +--- Forum: Fasihi simulizi (https://jifunzekiswahili.co.tz/forumdisplay.php?fid=6) +---- Forum: Ushairi (https://jifunzekiswahili.co.tz/forumdisplay.php?fid=50) +---- Thread: SHAIRI: MAMA (/showthread.php?tid=1061) |
SHAIRI: MAMA - MwlMaeda - 08-29-2021 MAMA Kifo kimeniadhibu, kukukosa wangu mama, Ona ninapata tabu, kutwa nimeshika tama, Naona Kama ajabu, furaha ilivyozima, Japo siku zimepita, ninaona Kama juzi. Kifo hakina adabu, daima chatuandama, Na sasa upo ghaibu, ewe binadamu mwema, Kusahau sijaribu, hata ningeshikwa homa, Ningelikuwa mjuzi, mama ungelirejea. Kuswali nilijaribu, wenda kifo kingekwama, Ilipodhidi ghadhabu, kikakuchukua mama, Hapo ulikuwa bubu, huwezi tena kusema, Nikatiwa ukiwani, kwenye dhiki na madhila. Dunia kuniadhibu, kumbe haina huruma, Nikambulia adhabu, shida zikanisakama, Ukiwa ndio sababu, dunia haina jema, Kweli ukiwa kidonda, amini habari hizi. Nilitiwa majaribu, nusula niwe kilema, Nayo maneno ya gubu, moyoni yaliniuma, Haki nilipata tabu, niamini wangu mama, Duniani Kuna watu, na Mimi nimetambua. Naona nishike nibu, nikuandikie mma, Ingawa hutanijibu, najua utausoma, Basi nikaona hebu, nikutakie salama, Nakumbuka tuvyopika, pamoja tukapakua. Akwepushie adhabu, mamangu ulale pema, Na siwezi kujitibu, nikakusahau mama, Kwangu hili ni jaribu, kuondoka limegoma, Ninakukumbuka mama, daima dumu dawamu. Beti chache zanisibu, nikuage wangu mama, Kuacha Nina sababu, chozi linaniandama, Majonzi yamenisibu, nalia bila kukoma, Baibai mama yangu, nakukumbuka kipenzi. Mtunzi Filieda Sanga Mama B Mabibo Dsm 0753738704 |