SHAIRI: MANARA KARIBU YANGA - Printable Version +- JIFUNZE KISWAHILI (https://jifunzekiswahili.co.tz) +-- Forum: My Category (https://jifunzekiswahili.co.tz/forumdisplay.php?fid=1) +--- Forum: Fasihi simulizi (https://jifunzekiswahili.co.tz/forumdisplay.php?fid=6) +---- Forum: Ushairi (https://jifunzekiswahili.co.tz/forumdisplay.php?fid=50) +---- Thread: SHAIRI: MANARA KARIBU YANGA (/showthread.php?tid=1009) |
SHAIRI: MANARA KARIBU YANGA - MwlMaeda - 08-25-2021 * * *MANARA KARIBU YANGA** Wahenga walitwambia, Kimfacho mtu chake Hilo naomba tambua, kasahau dhiki zake Fungu jema kachagua , kubeba virago vyake Manara karibu ! Bora kufa masikini, Kuliko hizo fedheha Simba hawakuthamini, Mbwembe na yako madaha Ujira wako thumuni , wakakunyima furaha Manara karibu! Mbwembwe za mitandaoni,Wewe ziba masikio Wajue upo kazini,waisubirie shoo Hao ni malimbukeni Waone kama minyoo Manara karibu! Katika hii dunia, Mkamilifu ni Mungu Wao pia namakosa, Tena waache Majungu Wanapaswa kutulia ,wasijitie miungu Manara karibu! Yanga twakukaribisha , jione upo nyumbani Thamani kutokushusha , japo metoka jirani Bendera kupeperusha , Hilo tunaliamini Manara karibu! Dinna Minja ( Mom JADEN ) 0713 747414 AR❤️ |