SHAIRI: HACHINJI BATA - Printable Version +- JIFUNZE KISWAHILI (https://jifunzekiswahili.co.tz) +-- Forum: My Category (https://jifunzekiswahili.co.tz/forumdisplay.php?fid=1) +--- Forum: Fasihi simulizi (https://jifunzekiswahili.co.tz/forumdisplay.php?fid=6) +---- Forum: Ushairi (https://jifunzekiswahili.co.tz/forumdisplay.php?fid=50) +---- Thread: SHAIRI: HACHINJI BATA (/showthread.php?tid=1001) |
SHAIRI: HACHINJI BATA - MwlMaeda - 08-24-2021 HACHINJI BATA Hili ninalokwambiya, lisijekupa utata, Yakupasa kutuliya, ili maana kupata, Ukiwa ni mpupiya, hautaambua hata, Mtu mpita na ndiya, hafai kuchinja bata. Ninenalo zingatiya, wenda ukawa mpita, Wakikuita kimbiya, na kataa katakata, Vichochoroni ingia, ukiona kona kata, Mtu mpita na ndiya, hafai kuchinja bata. Ela kuku ni sawiya, kuchinja usijewata, Tena nduu furahiya, kuku hanayo matata, Kuku hautakawiya, shida haitakukuta, Mtu mpita na ndiya, hafai kuchinja bata. Si kwamba nakutishiya, yakuwa bata ang'ata, ila bata hutumiya, kitambo roho kukata, Hivyo hutasubiriya, mambo yako utawata, Mtu mpita ndiya, hafai kuchinja bata. Kikomo nimefikiya, unyoya kando nakita, Najua wafikiriya, akili yabiringita, Shika nilokuhusia, kuchinja bata ni vita, Mtu mpita na ndiya, hafai kuchinja bata. Mshairi Machinga, mfaumehamisi@gmail.com, +255716541703/752795964, Dar es salaam, Kkoo. |