MyBB Internal: One or more warnings occurred. Please contact your administrator for assistance.
MyBB Internal: One or more warnings occurred. Please contact your administrator for assistance.
MyBB Internal: One or more warnings occurred. Please contact your administrator for assistance.
MyBB Internal: One or more warnings occurred. Please contact your administrator for assistance.
JIFUNZE KISWAHILI - MFANO WA TARIHI

JIFUNZE KISWAHILI

Full Version: MFANO WA TARIHI
You're currently viewing a stripped down version of our content. View the full version with proper formatting.
Kijana Kadenge ambwaga Jemedari Nyangumi
 
“Tuseme hii ndiyo hatima ya utawala wangu?” Alijiuliza Mfalme Ntire akiwa mwenye majonzi makubwa. Akatangaza katika milki yake kuwa yeyote atakayefanikiwa kumuua Jemadari Nyangumi atampa robo ya milki yake.
 
Wakatoka wanaume wa miraba minne, wakajaribu kupambana na Jemadari Nyangumi lakini wakateketea wote. Jemadari Nyangumi alikuwa anakaribia kabisa kuteka ardhi yote ya Mfalme Ntare.
 
Akatoka Kadenge kama walivyozoea kumwita. Miguu yake imeangalia kushoto na kulia. Macho yake ni madogo mithili ya macho ya mamba.
 
Akafika kwa Mfalme akamwambia, “Mtukufu Mfalme, naomba ruhusa yako nikamng’oe huyo nduli.” Mfalme akamjibu akasema, “Mfupa uliomshinda fisi wewe utauweza/” Kadenge akasema, “Nitauweza Mfalme Mtukufu.”
 
Mfalme akamwambia, “Nakuruhusu uende lakini siwezi kuruhusu jeshi langu kuongozana na wewe maana ni aibu tupu,” Mfalme akasema huku akibinua mdomo. Kadenge akatoka akachukua jiwe lililokuwa katika kombeo lake akamwendea Jemadari Nyangumi. Jemadari alipomwona akacheka, akasema, “Wewe ndiyo nani? Jeshi huna, silaha nazo huna, njoo uone. Nitakuvunjavunja mbavu zako a nyama yako itakuwa chakula cha tai.” akasonya huku akisogea mbele kwa mikogo.
 
Kadenge akamwangalia, akarusha jiwe lililokuwa katika kombeo lake, likamgonga Jemadari Nyangumi kwenye paji la uso; akaanguka chini puu! Damu zikaanza kumtoka mithili ya maji ya bomba. Mwisho akaaga dunia.
 
Askari wa chini yake walipoona Jemadari amekufa, wakakimbia. Watu wote katika ufalme wa Ntare wakashangilia, wakambeba Kadenge mpaka kwa Mfalme.
 
Mfalme akafurahi, akamgawia Kadenge nusu ya ufalme wake, wala siyo robo. Watu wote wakafurahi sana. Mzee mmoja akasikika akisema, “mdharau mwiba mguu huota tende.”