MyBB Internal: One or more warnings occurred. Please contact your administrator for assistance.
MyBB Internal: One or more warnings occurred. Please contact your administrator for assistance.
MyBB Internal: One or more warnings occurred. Please contact your administrator for assistance.
MyBB Internal: One or more warnings occurred. Please contact your administrator for assistance.
JIFUNZE KISWAHILI - SIMULIZI : “JENEZA LA AJABU ” **SEHEMU YA 11*

JIFUNZE KISWAHILI

Full Version: SIMULIZI : “JENEZA LA AJABU ” **SEHEMU YA 11*
You're currently viewing a stripped down version of our content. View the full version with proper formatting.
SIMULIZI : “JENEZA LA AJABU “
**SEHEMU YA 11*
Msitu wa majini;
Giza likiwa tayali  limeshaingia, hali ya ukimya iliweza kutawala sana katika msitu. Kwani viumbe wengi wa msituni walikuwa tayali wamejipumzisha, isipokuwa katika ngome ya malikia, kwani ndege pamoja na wadudu waliendelea kuruka ruka na kuimba nyimbo nzuri sana, wakifurahia uwepo wa maua yale ya kupendeza katika ngome ya malikia. Nyuki nao hawakutaka kuwa nyuma, waliendelea kuruka katika maua yale, na kisha kufyonza maji yake ili wakapate kujitengenezea asali.
Ndugu msomaji,kijana hodari Njoshi akiwa amesimama  kama sanamu,tena kama sanamu lile la kariakoo, katika duka la nguo la muhindi baada ya kukanyaga maji ya ajabu bila kujitambua. Aliendelea kuzungusha macho yake huku na kule, akitazama maua yale ya kupendeza.Huku harufu nzuri ya maua ikipenya katika matundu yake mawili ya pua yake, na pia sauti nzuri za ndege zikisikika katika masikio yake na kumfariji Njoshi. Bila kujitambua alijikuta akisahau machungu yote ya msituni na kujikuta akitabasamu, kwani ndege wale walimfurahisha sana.
“Aiweeeh mtukufu Gutamanya, kumbe ni wewe kijana, adui wetu wa msituni, kijana mzuri kiasi hiki, kwa nini umewaua ndugu zetu “,ghafla sauti nzuri na nyororo ilisikika na kumshitua Njoshi, kwani mawazo yake yalikuwa mbali sana, tena katika dunia nyingine wakati akiwatazama ndege wazuri katika ngome ya malikia na kusababisha ajisahau kuwa alikuwa katika hatari. Sauti hii nyororo iliyosikika, haikuwa nyingine bali ilikuwa ni sauti ya malikia. Baada ya kufika katika geti la ngome yake, na kumkuta Njoshi akiwa amesimama huku akiwa kashikilia panga lake, panga ambalo asingeweza kulitumia tena, kwani tayali alikuwa hawezi kutoka mahali alipo.
Malikia alitokea kumpenda Njoshi mala baada ya kuitazama sura yake, kwani alikuwa ni kijana mzuri sana huku weupe aliokuwa nao ukimpendezesha zaidi na zaidi. Malikia akiwa anatazama kifua cha Njoshi, kifua ambacho kilionekana kuwa cha mazoezi na kusababisha sehemu za tumbo lake kujikata kama pingili, malikia alijikuta hasira alizokuwa nazo zikimtoka na kisha kumuulza Njoshi maswali, tena kwa upole hali ambayo iliwashangaza majini wengine akiwemo jini mweupe aliyekuwa amesimama nyuma ya malikia, na kufuatiwa na kundi kubwa la majini waliokuwa wamebeba siraha za kila aina, ikiwemo mishale pamoja na mikuki ya ajabu.Mishale hii pamoja na mikuki ilikuwa ni tofauti na ile ya binadamu, kwani ilikuwa na uwezo wa kumpiga adui na kumgeuza kuwa kiumbe yoyote yule kama walivyotaka, unaweza kugeuzwa nyoka au hata ndege na kisha kukamatwa na kukufungiwa katika banda lao dogo walilolitumia kwa ajili ya kuwafungia binadamu wote waliouvamia msitu na kisha kuwapatia mateso makali.
“Aiweeeh malikia wa msituni, sikukusudia kuwaua ndugu zako, niuwie radhi malikia ” ,Njoshi alijitetea huku mmoja wa majini akimnyanganya Njoshi panga pamoja na kumvua kitambaa cheusi alichokivaa kiunoni. Baada ya kumnyanganya vitu hivyo, hakuwa na siraha yoyote ile ya kumlinda kwani walikagua begi lake jeusi alilolivaa mgongoni na  hawakukuta kitu chochote, kwani begi hilo lilitumika tu kuhifadhia panga pamoja na kitambaa kile cheusi.
Baada ya kuamini kuwa Njoshi asingeweza kuwadhuru. Malikia alimzunguka Njoshi mala tano, huku akitamka maneno ya ajabu, maneno ambayo mimi na wewe hatujui, kwani viumbe wale walizungumza kila lugha waliyoitaka wao, kwani hawakuwa binadamu bali majini, viumbe hatari sana.
“Ihiii………iwii……hii……”,malikia alizidi kutamka maneno ambayo waliyatumia kupiga kelele pale walipokuwa wana hasira na kuugulia maumivu, kipindi ambacho ndugu zao wameuawa huku akizidi kumzunguka Njoshi, na alipomaliza mzunguko wa tano Njoshi aliweza kuzinduka
“Umefuata nini katika msitu huu, ewe mtoto wa Nyangoma “,malikia aliongea huku moyo wake ukiwa tayali umempenda Njoshi kimapenzi, na kujuta maneno ya laana ambayo tayali alitakiwa ayakimilishe, jambo ambalo lilianza kuwa ngumu kwani tayali alikuwa ameshampenda Njoshi mala baada ya kuiona sura yake.
“Nimefuata utajiri, “,Njoshi akiwa anajalibu kujinyosha huku akitupa mikono yake huku na kule akiwa haamini kama kweli ametoka katika mtego ule, mtego ambao ulimfanya asimame kama sanamu bila kutikisika. Aliweza kujibu swali la malikia na kumdanganya kwani msituni alifuata jeneza la ajabu pamoja na fimbo ya kifalme na wala sio utajiri.
Msema ukweli ni mpenzi wa mungu, na pia ukweli siku zote utakuweka huru. Malikia pamoja na majini wote walikasirika sana kwani walichukia uongo kuliko kitu chochote kile, bola uwaue kuliko kuwadanganya.
“Hebu mkamateni, mkamfunge kwenye mti wa mateso “,Malikia alitoa amli Njoshi akamatwe kwani hisia za mapenzi zilitoweka ghafla, baada ya Njoshi kuwadanganya, bila kutambua kuwa majini hawadanganyiki, walikuwa na uwezo wa kutambua chochote kile bila kuambiwa na mtu yoyote.
Haraka sana askari wa msituni wakiwa na hasira sana na Njoshi, kwani aliwaua ndugu zao. Walimchukua Njoshi na kisha kumfunga katika mti mrefu, mti wa ubuyu uliopatikana katikati ya ngome ya malikia. Mti huu uliitwa mti wa mateso, kwani wadudu wakali kama siafu na nge wenye sumu kali, walipatikana katika mti huo na kumuadhibu kila aliyefungwa mahali hapo.
“Aiwee…eh mizi…mu ya mababu nakuf…aaa!! ” ,Njoshi alipiga kelele huku maumivu makali akiyasikia, kwani baada ya kufungwa katika mti huo. Siafu pamoja na nge wengi walimtapakaa mwilini na kumshambulia, huku viumbe wote wa msituni wakicheka kwani waliamini tayali kisasi chao kilikuwa kimefanikiwa.
Tofauti kabisa na malikia, hakuwa na furaha kabisa kwani alitokea kumpenda Njoshi ,hivyo ilimbidi afanye hivyo kwani Njoshi alionekana mbishi na mwenye dharau, baada ya kumdanganya.
“Utakaposema ukweli, sababu iliyokuleta msituni, ndipo utatoka mahali hapo ” ,malikia aliongea huku akijiamini, maneno ambayo Njoshi hakuweza kuyasikia kwani tayali alikuwa amepoteza fahamu.
Ikulu kwa mfalme;
        Watu walishindwa kupata usingizi katika ngome ya mfalme, tofauti kabisa na siku zingine. Waliendelea kulia huku wakiwa wameketi, wamekizunguka kitanda ambacho kulikuwa na maiti ya mfalme iliyokuwa imefunikwa kwa shuka zuri jeupe, huku sehemu ya kichwa chake ikiachwa wazi.
Wake kwa waume, ndugu pamoja na vijakazi wa mfalme, hawakusitisha sara zao kwa mizimu ili siku inayofuata Njoshi aweze kurudi na jeneza kutoka msituni. Bila kutambua kuwa Njoshi alikuwa tayali ameshakamatwa, na alikuwa anapatiwa mateso makali.
“Eeeh mizimu ya mababu, mrudisheni Njoshi wangu salama “,binti mfalme Grace, mpenzi wake Njoshi, yeye aliendelea kulia huku akijuta kumruhusu kipenzi chake kwenda msituni..kifo cha baba yake japo kilimuumiza lakini baba yake hakuwa muhimu sana katika maisha yake kama alivyo Njoshi. Aliamka kutoka katika kiti chake alichokuwa amekalia sebuleni, kiti kizuri kilichotengenezwa kwa miti na kisha kuelekea chumbani kwake na kuwaacha ndugu zake wakiwa wanaendelea kuhuzunika huku wakiutazama mwili wa mfalme,ambaye tayali alikwishakufa.
Mwamutapa;
       Mama yake Njoshi anaota ndoto ya ajabu,anaota kuwa Njoshi akiwa msituni alienda kuoga katika mto uliopita katikati ya msitu.Akiwa anaogelea,Mamba aliweza kumwona Njoshi na kisha kumkimbiza.Kutokana na Njoshi kuchoka sana na safari  ndefu msituni,alichoka kuogelea haraka kumshinda mamba yule na kujikuta akitafunwa na yule mamba.
“Aiweeeh ……mizimu ya mababu mwanangu yuko hatarini,muepusheni na balaa”,mama yake Njoshi alikurupuka kutoka usingizini,na kisha kumuombea mwanae kwa mizimu iweze kumlinda kwani aliweza kuota ndoto ya kutisha,ndoto ambayo alimaanisha Njoshi alikuwa katika hatari kubwa.Kwani kitendo cha Njoshi kutafunwa na mamba katika ndoto,kilimaanisha hatari kubwa iliweza kumkabili Njoshi usiku huo,usiku wa kuamkia siku ya jumatano.Bila shaka mama yake Njoshi alikuwa sahihi kabisa,kwani usiku huo mwanae alikuwa amefungwa katika mti wa mateso msituni,huku akiliwa na siafu pamoja na nge wenye sumu kali.Mateso haya yalikuwa makali sana na kupelekea Njoshi kupoteza fahamu.