MyBB Internal: One or more warnings occurred. Please contact your administrator for assistance.
MyBB Internal: One or more warnings occurred. Please contact your administrator for assistance.
MyBB Internal: One or more warnings occurred. Please contact your administrator for assistance.
MyBB Internal: One or more warnings occurred. Please contact your administrator for assistance.
JIFUNZE KISWAHILI - SIMULLIZI : MIMI NI MUAFRIKA ……SEHEMU YA 10…

JIFUNZE KISWAHILI

Full Version: SIMULLIZI : MIMI NI MUAFRIKA ……SEHEMU YA 10…
You're currently viewing a stripped down version of our content. View the full version with proper formatting.
…SEHEMU YA 10…
Msitu wa mikoko;
Mlio ya magari ulisikika, mwangwi ukasikika na kupenya sehemu zote za msitu wa Mikoko, Mpuzu akapanda juu kabisa ya mti wa ubuyu, alitaka kudhibitisha kama sauti zilizosikika zilikua za magari ya kikoloni,akiwa juu ya mti wa ubuyu, aliona msafara wa magari ya wazungu mia moja, kilomita takribani tano kutoka msituni, akashuka haraka juu ya mti, kuwapatia taarifa Waafrika wenzake.
“,Wanakuja, sio muda mrefu watakua mahali hapa,nazani wanawake na wazee wako mahali salama kwa sasa, lakini wanapaswa kutulia kimya, wasipige kelele, vijana kumi wenye silaha pandeni juu ya mti huu wa ubuyu, wengine pandeni kwenye miti mingine karibu na mitego ilipotegwa ……”,Mpuzu Yahimana aliongea, Angel alikuwa pembeni yake,vijana kumi wakapanda juu ya mti mkubwa wenye urefu wa futi mia moja kwenda juu, mti uliojaa matawi na kuficha Waafrika, wanawake, wazee pamoja na watoto.
Vijana na wanaume wa kiafrika wenye nguvu, wakapanda kwenye miti karibu kabisa na mitego waliyotega, kwa ajili ya mashambulizi. “,Unaenda wapi? baki utakufa, si salama tunapoelekea, “Mpuzu alimfokea dada yake Mwamvua, aliyetaka kuongozana nao, kwenda kupambana, mkononi hakuwa na silaha nyingi zaidi ya panga kubwa katika mkono wake wa kulia.
“,Siwezi kufa kirahisi,hata nikifa,nitakuwa nimekufa kishujaa,naenda kupigania uhuru wa nchi yangu…”,Mwamvua akiwa na nyuso isiyo na tabasamu wala furaha aliongea,alidhamiria kupambana kufa na kupona kupata uhuru wa nchi yake, haijalishi alikuwa na umri kiasi gani.
“,Let her go with us, she know how to fight, anajua kupigana, alipiga white people kule kwa great fort ,muache aende na sisi…”,Angel alimtetea wifi yake mtarajiwa, alishuhudia kwa mara ya kwanza Mwamvua alivyowatia adabu askari wa kizungu katika ngome ya wakoloni,siku mbili zilizopita,tangu siku hiyo alimuheshimu Mwamvua, msichana mdogo mwenye umri wa miaka kumi na tatu tu.
“,Sawa, twende, lakini kuwa makini, maana hujapona vizuri majeraha yako……”,Mpuzu aliongea, akamruhusu mdogo wake kuongozana naye, wote wakakwea miti,wakiwa na silaha za jadi isipokuwa Angel peke yake aliyekuwa na bastola mkononi, bastola aliyotoka nayo katika ngome ya wakoloni.
…………………………………
Jenerali Agustino Darwini aliongoza msafara, kundi la pili la askari mia tatu wa kikoloni,wakafuata njia ndogo iliyopita mkono wa kulia wa kibao chenye jina la msitu,wakaanza kuingia katikati ya msitu.Wakijiamini kwani silaha za Waafrika,silaha za jadi, hazikuwa na uwezo wa kufua dafu mbele ya silaha za wazungu, bunduki pamoja na miripuko ya mabomu.
“,Chochote kitakachotokea mbele ya macho yako,just kill, ua kuyakomboa maisha yako, bila hivyo jeshi lote litapata adhabu kutoka kwa gavana, hakikisha unarudi na kichwa cha Muafrika katika ngome kubwa……”,jenerali wa kikoloni, Agustino Darwin aliongea kwa kiswahili safi kabisa, akiwa mbele kabisa ya askari mia tatu wa kundi lake, macho yake yaliangaza mbele pamoja na msituni, akasahau kuangalia chini pamoja na juu ya miti, mahali walipojificha Waafrika.
Safari ilipamba moto,kundi la jenerali Agustino likaingia katikati ya msitu, macho yao yaliangaza mbele, pamoja na kona zote za msitu, wakapuuzia kuangalia juu ya miti, waliamini Waafrika wangejificha vichakani, mahali salama na vigumu kuonekana, kinyume kabisa na fikra zao, vijana hodari wa Kiafrika walikua juu ya miti ,wakiwaona vizuri askari wa kikoloni,wakijipanga namna ya kuwashambulia, wakawasubili wasogelee mitego yao, ili wawashambulie vizuri.
“,ooooh, help me!, help me!, nisaidieni ,…”,
“,Paaaa, paaaa, paaa …”,
“,Hel…p…me. …,nak…ufa ” ,
kelele zilisikika, jenerali Agustino alipiga kelele kuomba msaada,alijikwaa kwenye mtego wa kamba bila kutegemea, mguu wake ukaburuzwa na kamba mita kadhaa, askari wake wakashambulia bila mafanikio, gogo kubwa lilitoka juu ya mti na kutua katika tumbo la jenerali Agustino Darwin, damu nzito ikatoka mdomoni, mapuani na masikioni, jenerali wa askari wa kikoloni akafa palepale. Askari wake wakabaki wamepigwa na butwaa, kundi lote la askari wa kizungu wakashusha silaha zao mikononi mwao, wakausogelea mwili wa kamanda wao kuuchunguza. Wakiwa hawa amini kile kilichotokea.
“,Amekufa …”,
“,Yes, tayali amekufa, bastard Africans! “,
“,What this, wametuua sana,hii ni dharau, we must show them respect …”,
“,Foolish Africans, wapumbavu kabisa,tukiwakamata,there is no mercy…”,
Kundi la pili la askari wa kikoloni,kundi ambalo liliongozwa na jenerali Agustino Darwin,waliuzunguka mwili wa kiongozi wao,bila tahadhari yoyote,huyu alisema hili,yule akasema lile,bila kutambua uwepo wa maadui zao juu ya miti.
“,Pyuuu,pyuuu,pyuuu…”,
“,Yalaaa,am dying,nakufaa…”,
“,Pyuuu,pyuuu…”,
“,Aaaaaaah…”,
“,Run,run,kimbia,take your guns,shoot them,washambulie……”,
Ghafla kundi la askari wa kikoloni wakashambuliwa,zaidi ya askari kumi wakafa papo hapo,wengine wakafarakana,wakakimbilia msituni,kila mtu njia yake,hawakutambua mahali mishale iliweza kutokea,hawakufahamu mahali walipojificha maadui zao,ghafla mashambulizi yakasimama ,msitu ukawa kimya,kelele na vilio vya wakoloni ndivyo viliutawala msitu.
Askari wa kikoloni takribani ishirini walikimbilia mbele baada ya kushambuliwa, huku macho yao yakiwa bize kuangaza mbele yao, bunduki zao zilikuwa mikononi tayali kwa ajili ya kushambulia adui yoyote yule, hawakujua mahali walipokuwa wanakimbilia kama kulitegwa mitego, pia kulikuwa na askari wa Kiafrika wakiwa wamejiandaa kwa ajili ya kufanya mashambulizi.
“,Go, go, songa mbele, usiogope,be strong …”,
“,don’t worry boss, tutakamata watu nyeusi yote …”,
“„Let’s move, kimbia, songa mbele …”,
Kundi la askari ishirini lilitangulia mbele, likawaacha wenzao nyuma, baada ya kushambuliwa, wengine wakauawa na wengine kutokomea msituni kuyaokoa maisha yao, baada ya kushikwa na taharuki mara tu baada ya kushambuliwa. Kundi likasonga mbele, kila mmoja akimtia moyo mwenzake, walijiamini, waliiamini rangi yao, wakawadharau Waafrika, waliamini lazima watalipiza kisasi na kuwakamata Waafrika,na kuwapatia adhabu kali ikiwemo kunyongwa na kazi ngumu za shambani bila chakula wala maji.
“,yalaaaa, fu…ck…you, foolish Afric…ans,naku…faa …”,
“,don’t move, msije, sima…m…a …”,
“,Puuuu …”,
“,Yalaa…aa, you ki…lled
us (mmetuua) “,
Ghafla askari mmoja aliyekuwa mbele akatumbukia ndani ya shimo, baada ya kukanyaga mtego, akapiga kelele huku akitukana matusi ya kila aina,mwingine tena akatumbukia shimoni, akapiga kelele, akawaonya wenzake wasimame mahali walipo, hawakusikia, wakasogea mbele bunduki zao zikiwa mikononi, walitaka kuwakomboa wenzao waliotumbukia shimoni, wakajikuta wanakanyaga mahali pasipo stahili, kundi lote la watu kumi na nane waliokuwa wamebakia wakatumbukia shimoni, wakapiga kelele za maumivu, visu vilivyokuwa vimetegwa shimoni vikawachoma choma,mwingine kifuani, mwingine tumboni, wakafa palepale, ukimya ukatawala tena ndani ya msitu.
…………………………………
Gavana Richald Robeni, mke wake malikia Magreth, askari mia tatu pamoja na baadhi ya viongozi wa kikoloni walipita upande mwingine wa msitu, upande wa kushoto ambao haukuwa na mitego yoyote iliyotegwa, isitoshe Waafrika hawakujificha katika upande huo wa msitu.
Gavana na kundi lake walisonga mbele, walikuwa makini sana, waliangaza pembe zote za msitu kwa umakini wa hali ya juu, silaha zilikua mikononi mwao, macho yao yaliangaza mita mia moja mbele, juu na chini, kushoto na kulia. Laiti kama wangepita upande wa kulia, mahali walipo jificha Waafrika,kwa umakini walio nao,bila shaka wasingepata madhara makubwa, pengine wangetambua mahali walipo jificha maadui zao.
“,Yala…aa, nakuf…aa, fuck you,……”,
“,paaa, paaa, paaa! “,
Ghafla gavana alisimamisha msafara, alisikia kelele na milio ya risasi upande wa pili wa msitu, hakuona haja ya kuendelea kusonga mbele.
“,let’s go back!,twendeni upande wa pili wa msitu, huko ndiko kuna maadui,”
“,listen, listen, they are shouting, wanapiga kelele mingi huko, wanashambuliana …”,
“,My daughter jamani,let them not kill my daughter, wasimuue mwanangu ……”,
Kundi lote liligeuka nyuma, kila mmoja alisema neno lake, baba yake Angel Richald Robeni aliwahofia askari wake kuuawa, mama yake Angel alihofu mwanae kuuawa, baada ya kusikia milio ya risasi na kelele za vilio, wote wakaanza kurudi nyuma wakikimbia, upande wa pili wa msitu.
…ITAENDELEA …
Usikose vita ya msituni,Waafrika na wakoloni wazungu, Itakuwaje?, usikose sehemu ijayo …