MyBB Internal: One or more warnings occurred. Please contact your administrator for assistance.
MyBB Internal: One or more warnings occurred. Please contact your administrator for assistance.
MyBB Internal: One or more warnings occurred. Please contact your administrator for assistance.
MyBB Internal: One or more warnings occurred. Please contact your administrator for assistance.
JIFUNZE KISWAHILI - SIMULIZI : CHOZI LA DHAHABU SEHEMU YA 07

JIFUNZE KISWAHILI

Full Version: SIMULIZI : CHOZI LA DHAHABU SEHEMU YA 07
You're currently viewing a stripped down version of our content. View the full version with proper formatting.
SIMULIZI : CHOZI LA DHAHABU           
 
SEHEMU YA 07
      Hivyo ndivyo namna sauti za abiria zilivyosikika,Nakweli mda huo tayari gari lile lilianguka hadi chini kabisa ambapo kutoka kwenye lami huko juu kuja chini ni mita  takribani nane.Kwakweli gari lile lilipoanguka abiria huko ndani wakawa wamechanganyikiwa kwelikweli kwa wale ambao wamenusurika kufa Ndiyo waliokuwa wakijionea ni namna gani watu walivyoumia.Abiria wachache waliojiweza Kwaujumla amabao Walikuwa na nafuu wakaanza kutafuta namna ya Kutoka.
       Kwa bahati nzuri na ni jambo la kumshukuru mungu Zamda na Tito wamenusurika kabisa ila ni makovu tu Kwa usoni na mikononi kwa ule mrushano tu.Yote hii ni Kwasababu kuna baadhi ya abiria ambao wameumia sana hao hawakuwa wamejifunga vizuri Mkanda. Kwahiyo Ndiyo maana wengine wakawa wamevunjika shingo,kuna mwingine hapo hapo kavunjika kiuno.
      Kwahiyo abiria waliobaki wakaanza kujinasua wakiwemo huyo Zamda na Tito wakiwa wanatokea kupitia sehemu ya kioo cha Mbele kwa dereva. Lakini dereva Anaonekana amefariki hapo hapo.Kwa ujumla mwili wake haufai kabisa.kwa ujumla dereva alikuwa ni mnene fulani Hivi hivyo Basi baada tu ya gari kuanguka na tumbo lake likawa limebanwa kwelikweli na usikano na kujikuta limepasuka.Kwahiyo dereva alikuwa hafai kabisa, Na bahati kuna gari Ambalo lilikuwa linatokea sehemu nyingine huko ili kuelekea Ngata likawa limeona kuhusiana na ajali hiyo iliyojitokeza hapo,Ndipo dereva akasimamisha gari na abiria wake karibu wote tu wakawa wameshuka. Yule dereva kwa usalama mzuri wa wale majeruhi ikabidi apige simu makao makuu ya polisi huko Ngata ili wafanyiwe msaada. Ilikuwa hivi.
     "Dereva kasimama pembeni ya Gari lake huku akiwa amejishikiza kwa mkono wa kushoto kwenye mlango wa gari lake akisema Hivi". Hallo
     Karibu hapa unaongea na kitengo ya masikilizo ya majanga ya mbali.Jieleze.
Hapa unaongea na dereva wa gari namba  K CBC 678 la kampuni ya SAKAS.COM
Mhhh jieleze.
Aaaa nilikuwa natokea Kimbu kuja Ngata Lakini nimefika hapa daraja la Kisisiri nimekuta kuna gari limepata ajali kubwa Sana Yaani Kwaujumla ni ajali mbaya sana.
Mmmh gari namba gani na kampuni gani?."Kwahiyo ikabidi dereva yule atoke pale alipokuwa amesimama na kuelekea  Mbele ya gari lililopata ajali ili aweze kuzisoma namba za gari Hilo na kule makao makuu wajue ni namna gani wafanye ili kuweza kuwapatia Msaada. Lakini Chakushangaza ndipo ile tu Dereva yule anakanyaga kama hatua nne hivi kwenda Mbele gari lililopata ajali likawa limelipuka na kuwaka moto lote kuanzia Mbele hadi nyuma. Jambo Hilo likamfanya dereva yule aliyekuwa anatoa taarifa kule makao makuu ya polisi ya kitengo hicho maalumu kukosa ushahidi Yaani namba za Hilo gari baada ya kulipuka na kuwaka moto lote.Dereva yule alipigwa na butwaaa kwelikweli na kushindwa hata ni namna gani aongeee.Akawa amenyamaza kidogo kwa sekunde kazaa kisha akasema Hivi".Mkuu Yaani mda huu gari limelipuka lote na  kuwaka moto Kwahiyo nashindwa hata nitaje nini Yaani.Kwasababu limewaka moto kuanzia Mbele hadi nyuma.
Haya kwani gari hilo limepatia ajali hapo darajani kabisa Au laa?.
Limepatia ajali hapa hapa Yaani ni kama hatua thelathini kutoka Kwenye daraja la Kisisiri na hili gari lilipopatia ajali.
Haya tunakuja mda si mrefu sasa Hivi. Pasije pakajitokeza mtu yeyote anayejifanya anatoa msaada hapo wa kuwachukua abiria na kuwapeleka hospitali.Kwasababu wanaweza wakawa si watu wema.
Sawasawa.
Kuwa makini Sana tunakuja Sasa hivi pamoja na waandishi wa habari.
Sawasawa.
Huku kwa Upande mwingine Zamda na Tito wanaonekana wako mbali kabisaaaa na Gari lile.Kwa Tito alikuwa ameumia kidogo sana.Sehemu ya pajani karibu na Sehemu zake za siri akawa ameumia sana .Lakini kwa Zamda hakuumia Sana. Sasa hapo Ndiyo wamesimama wanaanza kulalamika Hivi.
"Zamda akiwa anaonekana ameshika kichwa kwa mabegi yao yanavyoungua moto akiwa anasema Hivi".Eeeeeeee mungu eeeeee mbona tena gari linawaka moto.Mabegi yetu yatakuwaje Jamani Tito. Angalia ile sehemu tuliyoweka mabegi ndiyo Kama inamalizikia kuungua kabisa. Itakuwaje Sasa Tito.
Ndiyo hivyo Zamda Sasa tutafanyaje.Yaani hatuna la kufanya. Afadhali hata sisi tumepona,unaona watu wanavyokufa huko kama nini.Mimi hapa nimeumia kidogo hapa kwenye paja.Itabidi nikifika Nyumbani nipafanyiye kazi kidogo.
Duuu hili ni balaa kweli kweli,
Yaani hadi najuta sana.
Kwanini Tito ?.
Unajua kule kazini waliniambia kwamba tutasafiri kwa gari la kazini, Lakini Mimi nikawawekea mgomo Kabisa kwamba Mimi ntasafiri pekee yangu tu.Sasa ukichanganya na ule msala wa Jana hapo ndipo nilipochanganyikiwa kweli kweli nikasema hapa lazima tusafiri kwa basi siyo gari la kazini.
Ila Ndiyo Hivyo Tito,Huwezi jua Kwasababu ungeshangaa mmepata ajali na hilo gari lenu Mara mnafariki wote .Huwezijua nini mungu amekuepeushia.Ndiyo hivyo wenyewe watakuwa wamepita hata njia nyingine Kwahiyo hata halitawakuwata Hilo janga.
ila ndiyo hivyo kweli kazi ya Mungu haina makosa.
       Basi baada ya mda kidogo gari la zima moto likawa limeshawasili hapo huku likiwa linapiga makelele yake kweli kweli. Lakini pia tayari na Gari lingine linaonekana hapo likiwa linamadhuni ya kuweza kuwapeleka abiria waliopona Nyumbani kwao.waandishi wa habari kutoka vyombo mbalimbali vya habari wakawa wamewasili katika tukio hilo na kuanza kufanya mahojiano ya hapa na pale.Lakini pia magari ya kubebea majeruhi na maiti yakawa yapo hapo.Kwahiyo kwa mda huo wakawa wamejaa Kweli Kweli watu wa huduma ya kwanza wakiwa wanatoa Msaada kwa majeruhi na maiti ambazo nyingine zimeungua vibaya kweli kweli.Lakini pia kuna sauti ya tangazo inasikika kwa kipaza sauti ikiwa ni sauti ya askari wa huduma ya kwanza akiwa anasema Hivi.
     Jamani poleni na majanga yaliyowakuta hivi karibuni "Abiria iliwabidi wapokelee tu Kwasababu kuna wengine hata hawakuelewa kwamba huyo anayeongea ni nani.Akawa anaendelea kusema hivi".kwa abiria ambaye hajaumia hata kidogo atapanda gari Ambalo linaonekana pale Mbele la rangi nyekundu na bluu namba KCCB 876 ili muweze kupelekwa hadi stendi kuu ya Kimbu.
      Nakweli kwa abiria wote ambao Walikuwa wamefanikiwa kupona katika ajali ile wakawa wameingia katika gari Hilo ambalo wameelekezwa ili Sasa uwezekano wa kuelekea huko Kimbu uanze.Kwahiyo abiria mojawapo ni hao Zamda na Tito wakawa nao wanaingia ili waweze kupata mahali pakukaa.
   Hivyo basi kwa majeruhi na maiti Walikuwa wakiokotwa kweli kweli Hapo chini kwa namna kwanza gari lilivyokuwa limeshona.Watu wengine wanaonekana wameungua tu sura ila mwilini hawajaumia hata kidogo. Ila wegine Ndiyo Hivyo hata mahali pakuweza kuwashika hapaonekani.
          Msafara wa kuelekea Kimbu ulianza Polepole huku kila abiria aliyepanda hapo akiwa bado hajiamini kama kweli ameokoka katika janga Hilo la ajali. Kwasababu kuna wengine hata hawajaumia Bali ni wamepata tu maumivu kwa mbali kidogo tu.
      Inapofika mishale ya saa Kumi na mbili Jioni Yaani magharibi ile tayari gari ambalo Walikuwa wamepakizwa abiria ambao Walikuwa wamepona tayari likawa limeshatia matairi yake katika stendi kuu ya Mkoa wa Kimbu wakiwemo Zamda na Tito. Abiria walifurahi sana na kumshukuru sana dereva aliyewaleta salama hadi pale stendi. Kwahiyo wakaanza kushuka Pole pole japokuwa wengine bado wanaonekana wana mauchafu mauchafu ya wakati wakiwa wanajinasua kule katika ajali iliyowakuta.
     Basi Zamda na Tito wakawa wameshashuka na kisha Tito akiwa Hana mzigo wowote zaidi ya simu yake tu na hata Zamda hivyo Hivyo, wakawa wamesimama mahali Hivi wakiwa wanapeana muongozo kidogo.Ilikuwa hivi.
       "Mda huo Tito akiwa kamshika Zamda Mkono huku akiwa anamwambia hivi".Zamda hapa Ndiyo Kimbu kama ulikuwa unapasikiaga tu Basi ndiyo Hapa. Hii Ndiyo stendi kuu ya Mkoa wa Kimbu.
       Mbona kuna baridi sana Sasa ?!!.
     Ndiyo asili ya Kimbu ilivyo Hivyo, Kwakipindi kama hiki huwa kunakuwa na baridi tena kali sana hasaa wakati wa usiku Hivi Ndiyo kali kabisaaaaaaa.
      Ahaaaaa Hatari hiyo na Mimi sweta langu ndilo Hilo limeshaungua kulee.
Haina shida tutanunua mengine, usihofu. Sasa embu tuanze msafara wa kuelekea nyumbani, Embu hata tupande pikipiki moja hapa japokuwa ni Karibu hapa na nyumbani ila wewe twende tupande tu.Kwasababu Mimi nataka tufike hapo nyumbani mapema ili nikajue nini kitafuatia.Lakini niliwataarifu Jana kwamba nakuja leo.
OK Basi twende zetu.
Basi Nakweli wakawa wamepanda pikipiki moja na kuelekea hadi huko Nyumbani kwao,ambapo nyumbani kwao ni uswahili sana tena sana ambapo ukishangaashangaa sana kwa mishale ya saa Kumi na mbili na kuendelea wahuni wanakukaba na kukuibia Fedha. Mtaa anaoishi ni mtaa wa Loronjo.
Baada ya dakika chache wakawa tayari wameshawasili nyumbani kwao baada ya kushuka kwenye pikipiki kisha wakaanza kutembea kwa mguu hadi nyumbani.Kufika hapo kisha Tito akawa amegonga geti mda huo huko ndani wakiwa wanaangalia Runinga Kwahiyo ni makelele kwa Sana.Akaamua kugonga na kuita kwakusema Hivi.
Hodiiiiiiii "Kimya"
Hodiiiiiiii "Ikasikika sauti ya mdogo wake wa mwisho ambaye anaitwa shezi akisema Hivi".
Karibu, nanii?.
Tito."Basi huko ndani wakafurahi kwelikweli kwamba Tito karudi ila hawajui karudi na nini wala na nani.kisha shezi akawa amekuja kufungua geti na kukutana na Tito kweli Lakini cha kushangazwa ni kwamba yuko na msichana. Tayari Tito anaonekana anamkaribisha Zamda wakiwa wanaingia sebleni mama akiwa amekaa karibu kabisa na mlangoni.Tito katangulia kuingia kisha akamsalimia Mama. Ilikuwa hivi".
Shikamo mama.
Marahaba pole na Safari mwanangu.
Shukran Sana."Anayefuatia kumsalimia mama ni Zamda. Ikawa hivi"
Shikamo mama.
Marahaba "hakupokea Mkono wa Zamda Bali akawa amemuuliza swali bwana Tito". Tito nani huyu?.
" Tito akawa anajibu kwa kujing'antang'ata Kweli Kweli akijibu swali Hilo huku  akimwangalia zamda.Alisema hivi ". Mama huyu ni mfanyakazi wa ndani nimekuletea." Zamda akatamani aongee neno lolote lile baada ya Tito kusema vile ila akawa akaamua kufuata msemo usemao funika kombe mwanaharamu apite yaani akawa amenyamaza tu.Kisha mama Tito akasema Hivi ".
Kwani nilikwambia Mimi nahitaji mfanyakazi wa ndani?.
Ndiyo nimekuletea Sasa mfanyakazi wa ndani.