MyBB Internal: One or more warnings occurred. Please contact your administrator for assistance.
MyBB Internal: One or more warnings occurred. Please contact your administrator for assistance.
MyBB Internal: One or more warnings occurred. Please contact your administrator for assistance.
MyBB Internal: One or more warnings occurred. Please contact your administrator for assistance.
JIFUNZE KISWAHILI - SIMULIZI : CHOZI LA DHAHABU SEHEMU YA 06

JIFUNZE KISWAHILI

Full Version: SIMULIZI : CHOZI LA DHAHABU SEHEMU YA 06
You're currently viewing a stripped down version of our content. View the full version with proper formatting.
SIMULIZI : CHOZI LA DHAHABU           
 
      SEHEMU YA 06
 Ikiwa ni alfajiri na mapema Jogoo wa mjini wameshaanza kuwika kila kona wanakofugwa.Miadhana ile ya kuamshana nayo inaadhiniwa kila kona ya mkoa wa Ngata. Kwa Ngata ni mkoa ambao Kwakweli una waislam wengi Sana. Kwahiyo Kwa mda huo lazima kuwe na makelele ya kutosha ya muadhana. Kwahiyo kuwika kule kwa majogoo na sauti zile zikawa zinawapenya kweli kweli hao Zamda na Tito kwamba hawaamini kama Kweli kumekucha. Kwasababu wanajua kama Ndiyo pamekucha Basi na Msafara nao ndiyo huo umewadia.
          Lakini pia huko njiani kwa wale wafanyabiashara nao hawachelewi kwa mda wao maalumu ambao wameupanga wa kuingia masokoni kila mtu kwenda kuchakarika na kazi zake maalumu zilizompeleka hapo sokoni.Basi huko njiani makelele nayo kwamwe hayaepukiki kabisa.
      Basi ikiwa tayari ni saa kumi na moja na robo ni mda ambao tayari Tito na Zamda wameshajiandaa ili Sasa Msafara wa kwenda Kimbu uanze.Basi wakiwa wanaonekana wako hapo ndani wakiwa wamesimama godoro wamelikunja ili yule rafiki yake na Tito aje kulichukua Kwasababu ndilo lake.Mda huo wakawa na maongezi kabla hawajatoka ndani hapo.
        "Tito akiwa anaonekana amesimama karibu na begi la Zamda hali hiyo ikiashiria kwamba atakayebeba begi la Zamda ni Tito.Kwasababu begi Hilo ni zito kweli kweli kulikoni hata begi la huyo Tito.Tito kasimama huku kashika kiuno mithili ya mtu aliyetoka kucheza ndombolo mda si mrefu huku akimwambia Zamda Hivi". hili godoro yule jamaa ambaye nilikwambia kwamba alinipatia tu atakuja kulichukua pakishakucha Kwasababu anajuana hata na Hawa wapangaji wa hapa.Kwahiyo hata kama tukiacha mlango wazi haina shida.
       "Zamda akiwa amevaa dera lake la rangi ya  bluu yenye maua hivi ya rangi ya njano.Akasema". Sawa haina shida.
      Kwahiyo Zamda Sasa ndiyo msafara unaanza kuelekea huko Kimbu. Kuna vitu vingi huko vya kwenda kushangaa Kwahiyo utafurahi sana kuona Hayo mazingira ya huko ila sijui kama Utakaa kwa amani huko Nyumbani.
      Kwanini?.
       Mama yangu wewe.
     Ndiyo hivyo Mambo yameshajitokeza. Embu tuanze msafara bana hata usinichefue alfajir yote hii.
     Haya twendezetu.Mimi nabeba hili begi lako kwasababu ni zito na wewe unabeba hilo langu halina kitu tu huko.Ni nguo chache tu zipo huko.
      Sawa.
       Basi wakiwa wanaonekana tayari ndiyo msafara wanauanza wote wanatoka nje na wanarudishia mlango na ufunguo wakawa wameuacha kwa mama mwenye Nyumba hao wanatoka nje na kuanza kuelekea huko stendi.Njiani wanakopita wala hawakutani na pikipiki wala nini Bali wanakutana na watu tu  wanaokimbilia masokoni haswaa haswa wengi wao ni wanaume wanaenda kununua wengine madafu,nazi na mengineyo. Kwasababu kwa Ngata hivi ni vitu ambavyo kuuzika kwake ni rahisi Sana.
      Ikiwa tayari kumeshapambazuka kidogo  wale watu wa kwenda msikitini nao tayari wengine ndiyo wanarudi baada ya kumaliza kuvuta uradi wa asubuhi na wengine bado huko wanaendelea kuvuta uradi.Kwahiyo na mda huo ni mda ambao baba Zamda naye anaonekana yuko na kanzu yake nyeupeee peee na ukichanganya na urefu wake anakuwa kama vile Mtoto wa Jini.Mda huo Baba Zamda akiwa anatoka msikitini huku akiwa na tasubihi yake akiendelea kuvuta uradi tu polepole bakora yake anaitumia kwa Mkono wa kulia. Basi akiwa anatembea na bakora ile hutembea kiushekhe kwelikweli kwa kunesa nesa mithili wa mfalme wa himaya fulani Hivi.
      Mda huo anaonekana Tayari yuko Nyumbani hapo akiwa na mama Zamda alikuwa na maongezi kidogo ya hapa na pale Kwakawaida ya mke na mme wanaopendana kwelikweli hivyo ni vitu ambavyo haviepukiki.Kwasababu baba zamda alipokuwa akitoka msikitini kamkuta hapo mama zamda kama anahudhuni kwelikweli.Kwamba yote hiyo ni kwasababu ya Zamda kuchukuliwa kirahisi tu na mtu ambaye hakutarajia kwamba kweli itatokea.kwahiyo ndiyo maana baba zamda akaamua kuongea naye kwa umakini.Alikuwa na maongezi kama ifuatavyo.
        " Akiwa bado hajavua kanzu yake huku nayo tasubihi akiwa ameishikilia huku kaegemea bakora yake akisema Hivi ".Sasa mama Zamda Hapa hata ulie Vipi ndiyo tayari Mambo yashakuwa Mambo.Waswahili Wanasema maji yakishamwagika hayazoleki na katika vitabu vya dini tulivyovisoma vinasema kwamba kila jambo linalomkumba Au kumtokea mwanadamu basi jambo Hilo alitambue kwamba jambo hilo limepangwa na Allah na yeye ndiye muamuzi wa yote.Yawezekana amepanga hivi tukawa tunalalamika sana kumbe kina kuna faraja yatwijia hapo mbeleni bali hatujui.Mungu hajatuwezesha upeo wa kuona kesho bali ametuwezesha upeo wa kufikiria kesho.Mama Zamda Hapa tungesema kwamba tumshike huyo mkaka wa watu ni Sawa angeenda jela ila Lakini Mimi hapa uso wangu ningeuficha Wapi Kabisaaaaaaa mtoto wa mzee wa msikiti kapata mimba akiwa bado hajaolewa.aibu iliyoje kwangu hiyo?.Hata kama tukiachana na habari ya kuaibika hapa nani angemlisha chakula,Wakati Maisha yetu ndiyo Hayo maisha ya kuunga unga tu.Bora waende wote huko Huko. Kwasababu Zamda ni Yeye mwenyewe ndiyo kaamua kuyaharibu maisha yake.Angalia kwasasa ndiyo Alikuwa anasubiria matokeo ya kidato cha pili. Sasa elimu gani aliyonayo hii,si sawa na mtu aliyeishia darasa la saba tu.Kwa ujumla Zamda ameona kwamba Yeye atafaulu Kwenye Mtihani wa mapenzi basi wasahisaji tulikuwepo makini saaaana moja wapo ni Mimi ndiyo  maana nimempa alama nzuri ya kusema wewe umefaulu kwenye mapenzi Sasa nenda kayafanye huru Hayo mapenzi. Mbona kiurahisi tu mtoto mdogo hivi aanze kuniumiza kichwa miyee,Lahasha ,Hapana. Mimi...mimi ni mtu mzima siwezikuaibika  kirahisi rahisi tu Hapa.Japokuwa kuna vingi tumevipoteza kama vile mahari hatutapata tena mahari,Kwasababu hapa ni mtu kauziwa tu mbuzi kwenye mfuko.Yaani laiti ndiyo hajapewa mimba wallah yule mtoto asingechukuliwa hapa bila millioni na kitu hivi.
           "Mda huo anaonekana mama kakaa hapo mlangoni kajikunyata Kweli Kweli huku akiwa kichwa kainamisha chini akiwa anamsikiliza kwa makini baba Zamda akiongea mithili ya mchambuzi wa mpira.Mama Zamda naye kwa mda ule akaamua kutoa lake la moyoni akisema Hivi" Ni Sawa mume Wangu Yaani mwanetu alikuwa bado mdogo sana na kama ni hayo mahari unayoyaongelea Kwakweli hata tungejikomboa na huu umasikini.Ila Sasa ndiyo hivyo maji ya moto yameshakuwa baridi, na watu huwa wanapenda kwenda kuangalia na kulipia bei ghali milima yenye barafu lakini njo sikia kwamba Barafu imeyeyuka yote hapo mlimani na kuanza kububujika unadhani kuna mtu yeyote atakayejihangaisha Hapo kuja kupanda tena huo mlima Lahasha."Mda huo baba Zamda Anaonekana akichukua kigoda kilichopo karibu naye hapo ili aweze kukikalia huku mama Zamda akiwa anaendelea na maongezi"".Bali utabaki kama historia tu kwamba palikuwepugi na mlima wa barafu hapa alafu baadaye barafu iliyeyuka yote ndiyo maana mto kwa Sasa.Sasa chungu chetu ndicho hicho kimechukuliwa bure bureeeee kwa macho yetu mawili tunajionea.Yaani sijui huko mtaani rafiki zake sijui watasemaje kwanza."Akawa amenyamaza na kama machozi yakiwa yanataka kuanza kumtoka kisha baba Zamda akawa anasema Hivi ".
      "Mda huo akiwa amekaa kwenye kigoda akiwa amemsogelea mama zamda kwelikweli huku maongezi akiyanogesha". Sasa mke wangu hata ulie machozi ya chuma ndiyo hivyo Mambo yashakuwa hivyo na ndivyo ilivyopangwa.Kwa ujumla iko hivi mzigo uliotwika kwa mtu fulani kwa kutwishana lazima pia utuliwe kwa kutuwana hata ikiwezekana yule mtwikaji inabidi atoe maelekezo ni namna gani ya kuutua huo mzigo japokuwa atakayeumia sana ni yule mtwishwaji japokuwa mwanzoni Walikuwa wakifurahi sana wakiwa wanatwishana Lakini mmoja Ndiyo anajulikana anafanya kazi hivyo ya kutwisha.Ndivyo ilivyo tu hivyo.Mambo mengine ndiyo hivyo tumuachie tu Mungu.
       Basi mda huo mama na baba Zamda baada ya kumaliza maongezi wakawa wanatawanyika huyu kaingia Jikoni kwa vinywaji vya asubuhi Baba Zamda kaingia ili avue kanzu yake na avae Sasa nguo za kazi Kabisa na mama Zamda akishamaliza hapo naye aende huko katika shughuli zake za kijungu Jiko kama kawaida yake.
      Kwa ufupi kijana Tito ni Kijana ambaye kwao katika familia yao kwa Yeye ndiyo wa pili na ndiye mvulana pekee katika familia yao.Ambapo mkubwa wake ni Mwanadada ndiye wakwanza ndipo akafuatia Tito.Kwaujumla katika familia yao Mama Tito amejaaliwa kuwa na watoto wake wa halali wanne.Ambapo wa kiume ni mmoja tu ambaye ni Tito.Wakwanza ni Bite, wa pili ni Tito ,wa tatu ni Soni na Wa nne ni shezi.Tito aliweza kusoma kuanzia darasa la Kwanza hadi darasa la Saba katika shule ya msingi Meziwa ambayo ilikuwa ni shule kwa kipindi hicho cha enzi za wakoloni ilikuwa iko chini ya wahindi.Yaani katika shule hiyo ni watoto wa kihindi tu walikuwa wakisoma hapo.Lakini baada ya kupata Uhuru ndipo nchi ya Kinani ikawa imeamua kujiunga katika Ujamaa mnano miaka ya 1960.Kwahiyo baada ya kuingia katika Ujamaa ndipo makampuni yote ya watu binafsi yakataifishwa na shule hiyo ya Msingi Meziwa ikawa chini ya serikali ya Jamhuri ya Kinani.Basi Tito alipofika kidato cha Saba na akawa amefanya mtihani vizuri tu na matokeo yake yakawa yametoka vizuri Sana ikabidi apelekwe shule za ufundi na vipaji maalumu. Lakini alipofika kidato cha pili masomo yakamshinda ndipo akamwambia mama yake kwamba anataka kwenda VETA Yaani The Vocation of Education and Training Authority iliyopo katika mkoa wa Kimbu kwaajili ya kwenda kusomea Au fani yake aliyokuwa anaipenda.Kwahiyo Tito akawa ameishia kidato cha pili kama Hivyo hivyo mchumba wake ambaye ni Zamda. Baada ya kumaliza VETA ndipo akawa amejaaliwa kupata kazi ya ujenzi wa barabara katika kampuni moja hivi ya wachina
      Basi tayari msafara wa kuelekea huko mkoani Kimbu kwa Zamda na Tito ukawa tayari uko Njiani Yaani ndiyo tayari wanaelekea huko Kimbu. Ikiwa ni mishale Ya saa saba mchana gari walilokuwa wamelipanda Zamda na Tito Kwakweli kama ni njia lilikuwa limeshika njia kweli kweli. Mwendo uliokuwa kwa mda ule ni mwendo ambao ni wa barabara za Haraka kweli kweli. Huko nje jua linaonekana limewaka kwelikweli.Ndani ya gari humo Joto limewazunguka kwelikweli abiria nao wakiwa wamejaa kwelikweli. Kwasababu Kipindi hicho ni Kipindi ambacho ni cha  sherehe za Mwisho wa mwaka nazo zilikuwa zimewadia.Kwahiyo ndiyo maana watu Walikuwa ni wengi sana wakiwa wanaenda Nyumbani kwao kusalimia kwa likizo fupi walizozipata,wengine kwa Ndugu zao.Kwasababu sherehe kubwa iliyowafanya watu wasafiri sana ni sherehe ya Christmas. Kwahiyo watu wakawa na hamu sana ya kwenda kuwasalimia Ndugu zao katika maeneo mbalimbali.
        Basi mda huo Zamda na Tito wanaonekana wako wamekaa siti moja mabegi yao wakiwa wameyaweka huko kwenye Boot ya Gari. Kwahiyo kwa mda huo Zamda na Tito Walikuwa na kama maongezi Hivi. Zamda anasema Hivi.
       Hapa tulipo Sasa panaitwaje?.
      Hapa panaitwa Kisisiri.Yaani hujawahi kupafika huku?.
      Nisafiri nasafiri naenda wapi Sasa Wakati Mimi ni Ngata tu Kwaujumla shuleni kwetu tu nimesharudi nyumbani.
Kwahiyo hata hujui historia ya hapa Kisisiri?.
 Siijui kabisaaaaaaa. Ni  mbaya sana Au
 Ndyo,ni mbaya sana.Kwasababu kuna sehemu hapo Mbele kuna kona hapo Ndiyo kama tunakaribia kuimalizia Kisisiri,kuna daraja liko hapo wanaliita daraja la Kisisiri kila aliyesafiri kwa njia hii atakuwa analijua historia yake na maajabu yake ya Ukweli.
Kwanini?.
Lina historia mbaya sana.
Mbaya!!??.Historia mbaya gani Hiyo.??.
Ya kuua.
Haaaaaaa yakuua tena,Mungu wangu Tusaidie hii Safari.
Ndivyo palivyo Hapa Kisisiri. Yaani kutokea ajali ni kitu cha kawaida ambacho kuanzia madereva na watu wengine wanajua kabisaaaaaaa.
Mbona wanitisha?. kwani kipindi kile ulipokuwa unatoka Kimbu kuja Ngata simulipita hapa mbona hamkuanguka?.
Hapana Mara nyingi ajali zinazotokea hapa ni kwa Yale magari ambayo yanatokea Ngata kwenda mikoa mingine na siyo yanayotoka mikoa mingine ya majirani na kuja Ngata. Kwahiyo Ndiyo maana sisi hatukukutana na hilo janga.
Daaaa Basi nasi yatupasa tumuombe mungu Sana.
Ni Kweli, ila jambo likishapangwa ndiyo hivyo Tena huwezi kulipagua na siku zote kazi ya mungu haina makosa Bali ya mwanadamu ndiyo iyakayoweza kuwa na makosa kama kuna wakosoaji.
Haya.
Basi mda huo dereva akiwa ameliivisha kweli kweli gari huku akiwa anafanya kama vile anataka  kuupunguza mwendo Kwasababu tayari wameshakaribia katika Hilo daraja la Kisisiri Ambalo linakona na baada ya kona kuna mteremko mkali Sana kila abiria hapo hufumba macho na kujifanya kama vile anaongea na malaika mtoa roho ili aweze kuwa na mazoea naye mapema sana.Dereva akiwa bado yuko katika Yaani si mwendo  mdogo wala mkubwa sana bali Kwaujumla ni mwendo kasi na Sehemu aliyopo barabara imependa juu sana Yaani hadi kufika chini yaani sehemu ya tambarare ni kama vile mita nane Hivi. Ghafla kwa Mbele dereva akaona kitu cheupe kwa Mbele kimesimama Kwaujumla alikuwa ni mtu akiwa amevaa nguo nyeupe aina ya kanzu.Mtu huyo anaonekana ni mrefu Kweli Kweli mweupeeeee na nywele zake zikawa zinaonekana ni ndefu sana kwakuwa hakuwa amezifunika na kitu chochote. miguuni hajavaa viatu Bali mtu huyo hajakanyaga chini Yaani yuko anaelea elea juu juu Usawa kama wa sentimita thelathini kutoka katika usawa wa ardhi. Ikiwa ameweka mikono kama picha ya yesu msalabani.Dereva alishika breki kwa Haraka na kujikuta tayari gari limeshapoteza njia.Sauti na vilio kwa abiria zikawa zinasikika tu huko Ndani ya gari
Uwiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiii
Yarabiiiiiiiii
Lahaulaaaaaaaaa
Laila hailallah.
Uwiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiii.