MyBB Internal: One or more warnings occurred. Please contact your administrator for assistance.
MyBB Internal: One or more warnings occurred. Please contact your administrator for assistance.
MyBB Internal: One or more warnings occurred. Please contact your administrator for assistance.
MyBB Internal: One or more warnings occurred. Please contact your administrator for assistance.
JIFUNZE KISWAHILI - SIMULIZI : CHOZI LA DHAHABU SEHEMU YA 01

JIFUNZE KISWAHILI

Full Version: SIMULIZI : CHOZI LA DHAHABU SEHEMU YA 01
You're currently viewing a stripped down version of our content. View the full version with proper formatting.
SIMULIZI : CHOZI LA DHAHABU
MWANDISHI: Saidi Kaita
SEHEMU YA 01
       Ni saa moja Jioni mda huo wakionekana mama na mwanaye aitwaye Zamda.Sehemu waliyokaa ilikuwa ni Jikoni wakiwa wanafanya Maandilizi ya chakula cha usiku.Jikoni hapo chakula ambacho kilikuwa kimebandika na kufunikiwa haki ilikuwa ni wali ambao ndio ulikuwa umedhamiriwa kuliwa usiku ule..Zamda kwa umri wake ndiyo ulikuwa ni umri wa tayari kufikia kuvunja ungo.Tangu akiwa mdogo ni mwana ambaye Kwakweli ambaye amejaaliwa uzuri ambao Kwakweli ni mungu amemjaalia.Basi mda huo mama Zamda akawa na maongezi kidogo na mwanaye Wakati wakiwa wanangojea wali uweze kuiva.Mda huo Mama Zamda akiwa amekalia kiti aina kigoda naye Zamda akiwa amekalia kigoda. Taa iliyokuwa ikiwapatia mwanga hapo jikoni ilikuwa ni taa ya kuchajisha kwa kutumia mwanga wa jua Yaani Solar Power.Hivyo  basi mazungumzo yalikuwa yanajikita sana katika suala la huyo Zamda kuvunja ungo.Kwahiyo mazungumzo yao yalikuwa kama ifuatavyo.
     Mwanangu Zamda ndiyo hivyo umeshakua. Utoto umekutoka na kwasasa umeingia kwenye usichana.Ambapo utoto huo ulikuwepo ni Kwasababu ya ukuzi wa mola namna ulivyo. Na kwasasa ndiyo Hivyo umeshakuwa katika makuzi mengine tena Yaani baada kuvunja ungo.Kuvunja ungo ndiyo mwanzo wa kuanza kuweza kujielewa Sasa ni tabia gani wewe kama msichana utakayokuwa nayo.Kwakweli mwangu kati ya watoto wangu ambao wananikosha roho yangu ambao kwaujumla nawategemea watakuja kniondoa katika haya maisha mabovu tunayoyaishi ni wewe.Najua iko siku na mimi ntaitwa mama mke na mtu ambaye anamiliki migari hiyooo.Yote hiyo ni kwasababu tu ya wewe mwanangu Zamda.Kwakweki mwanangu kwa uzuri umejaaliwa hadi natamani ningekuwa na hela ningeeajiri hata askari awe anakulinda tu na huyo askari awe ni askari wa kike mwenye nguvu ya kukulinda kwelikweli.Ila tatizo ndilo hilo sasa sisi mahoehae mungu ndicho alichotujaalia.Sawa Uzuri ndiyo huo umejaaliwa mwanangu ila Sasa Angalia Miluzi mingi humchanganya Mbwa. ""Zamda akiwa anamsikiliza kwa makini mama yake ilibidi amuulize swali kidogo kwa msemo ambao ameusikia kutoka kwa Mama yake.Alimuuliza hivi""
Mama Unamaanisha nini unaposema Miluzi mingi humchanganya Mbwa?."Alimuuliza kwa sauti ya chini iliyojaa aibu fulani kwa heshima anayompa mama yake.Mama akawa anamjibu kama ifuatavyo ".
Aaaaa....mwanangu japokuwa waswahili husema kwamba usimwambie mtu maana ya kitu fulani maana baada ya kumwambia maana hiyo tu atakuona hauna maana yoyote. Lakini kwa wewe kwa vile ni mwanangu hivyo basi nakupenda na pia nakutakia Maisha ambayo Kwakweli hata nikifa usiku wa leo hii maneno yangu haya yatakuwa yakisikika masikioni mwako.Macho yako yatakuwa yanavuta taswira ya namna tulivyokaa na taa yetu hapa.Nimesema kwamba Miluzi mingi humchanganya Mbwa mwanagu nikiwa namaanisha Kwamba"mda huo mama Zamda akawa amemgusa Zamda kwa Mkono wake wa kulia na Zamda akawa ametikisa kichwa chake akimaanisha ameetikia kisha mama Zamda akaendelea kusema  Hivi".Siku zote mbwa anapokutana na watu katika njia aliyopita na njia hiyo ikawa ni njia ambayo  imejaa watu wengi kila mtu anahulka yake.Basi wanaweza kila mtu akaanza kupiga mluzi wake kwa namna na madhumuni yake.Kuna ambao watapiga Miluzi kama vile wakipuliza Nai ,Wengine ndiyo hivyo kama sauti za chura wakiwa kati urojo wa maji asubuhi Au usiku ile wanatoa sauti zake.Lakini kuna wengine Nai watapiga hata makelele tu hata kama hawawezi kupuliza huo Mluzi.Lakini Mbwa Huyo mda huo Yeye hata jua kwamba haya ni makelele Au laa Bali atajua ni Miluzi ya watu wanaomtamani kumpiga .Basi mda huo Miluzi ile hupenya moja kwa moja hadi ndani ya masikio yake na kujikuta mbwa huyo anashindwa ni wapi pakuelekea.kinachomkuta hapo anaenda huku anarudi kule na huku tena mwisho wa siku kizunguzungu kinaweza hata kumpata.Basi hapo kumpiga Mbwa huyo ni kiurahisi sana...Sasa tena sana na kujikuta kaumia tayari."Zamda ikambidi aulize swali kwakuona maelezo ambayo mama yake anampa Kwakweli kama yana ukakasi kwake kidogo. Alimuuliza hivi ".
Sawa mama kidogo kama nakuelewa ila panaponishinda kuelewa ni kwamba kuna uhusiano gani kati ya Miluzi mingi humchanganya Mbwa na kuhusiana na Mimi kuvunja ungo?.Kwasababu... Sababu nahisi kama vile kidogo hapo sijakupata vizuri.Yaani nahisi ni kama Unataka kufananisha Biskuti na mkate ....mhhh sielewi mama Hapo.
Ni Kweli ni vigumu kuweza kunielewa kwa Haraka Bali yatakikana tafakuri kidogo ambapo Tafakuri hizo zitasindikizwa na maelekezo yangu ambayo nataka nikupatie.Ni kwamba mwanangu huyo Mbwa nimekutolea mfano wewe hapo japokuwa si kwamba wewe ni mbwa kweli."Zamda akacheka kwa sauti yake ya madaha kisha Mama Zamda akawa anaendelea na maongezi.""Yaani wewe kwasasa utakuwa ni mtu ambaye Kweli ukipita katika kundi fulani la wavulana kila mtu ataanza kukutamani na si kukupenda na siku zote mwanaume huanza kumtamani msichana na ndipo kama ni kumpenda ndipo ataanza kumpenda baada ya kukutana nae Mara kadhaa hivi.Sijui kama wanisikiiliza mwanangu kwa umakini?."Mda huo anapomuuliza hivyo akawa amemsogezea uso wake huku Mkono wake wa kulia tena akiwa anamshika Zamda kwa kuonesha usisitizaji fulani kwa mada anayoizungumzia. Zamda akasema Hivi"".
Mama nakusikiliza kwa makini Sana.
Hayaa nisikilize kwelikweli kwa makini.Mwanangu hii ndiyo dunia ya kipindi ya kizazi cha nyoka. Kwahiyo upitapo sehemu ambayo patakuwa na kundi la wavulana kila mvulana anaweza kukumezea mate tu na baada ya mda kila mtu ataanza Sasa kukutafuta kwa mda wake na hapo Sasa kila mtu huja na mluzi wake.Atafanya afanyavyo hadi mwisho wa siku utajikuta mluzi ule umekuchang'anya na kuanza kuukubali kwa asilimia mia moja kabisaaaaaaa na hata asilimia elfu moja inawezekana.Lakini baada ya hapo tena kesho pakikucha wataanza kuhadisiana huko magengeni utashangaa na mapema mwingine tena anakuja anaaza kukupulizia mluzi weeeeeeee kwa namna yake mwisho wa siku unaanza kuona Au unaanza kufananisha mluzi wa kwanza na mluzi wa pili upi umezidi.Kifuatacho kwa tamaa zako utajikuta waangukia kwenye mluzi wa pili.Hivyo hivyo mwisho wa siku unajikuta Miluzi imezidi na baada ya hapo wote waliokuwa wakikupigia Miluzi wakishajua wewe Ndiyo tayari huna muelekeo Kwasababu kule ukipigiwa Mluzi na mtu fulani waenda tu.Hapo Sasa wajikuta gazeti linachanika na wanunuzi na wasomaji hawana tena mda na hilo gazeti Ambalo lilikuwa likibamba Kweli Kweli likisema kwamba Zamda mashaalah Yaani hapo Ndiyo wewe sasa mwanangu hapo unakuta kila kona hawana hamu na wewe.Kwaujumla gazeti likishalowana hapo Kwakweli hata kama lilikuwa na mataarifa ya udaku chungu mzima wala hakuna anakayeanza kwenda kujihangaisha kununua vipande vya gazeti Hilo lililochanika kwa mvua iliyolinyeshea gazeti Hilo. Sijui kama wanipata Mwanangu?.
Fuuuuuuuuuuuuuuuuuu."Zamda akahema utafikiri kajitua mzigo fulani ambao ni mzito kwelikweli kwa maneno machache mama yake anayompatia Kisha akasema Hivi ". Kwahiyo mama Kwasababu mama Kwahiyo kukua Shida Tena?.
Mwanangu Hilo ni Jambo Ambalo Kwakweli linalohiitaji  kalamu ya kupigia msitari kabisa mmoja mnyoofu kabisaaaaaaa.Kukua nako ni mungu katujaalia sisi waja wake ili tuwe tunakuwa ni maelezo ya vipindi mbalimbali. Yaani kuna kipindi ulikuwa na mwaka sifuri hadi ukifikia miaka mitano,baada Hapo ukafikia hadi miaka kumi  na Sasa hadi leo hii Angalia umri wako.Kila kipindi cha umri wako kinakuwa na matukio ambayo yanawezakuwa mengine ni ya kufurahisha Au ya kuhuzunisha. Alafu mwanangu ukichanganya na huu umasikini tuliokuwa nao Kwakweli hapa nyumbani usijeukakufanya mwanangu kuanza kutaka kupata Hela za kujiremba kwakuuza mwili wako.
Sawasawa mama sitofanya hivyo nakuahidi.
Yaani mwanangu kwa hatua uliyofikia hii Kwakweli ni hatua ambayo kwa Mimi naona kama ni hatua ya kuhitaji kutumia akili sana.Kwasababu mwanangu kwasasa ndiyo upo hicho kidato cha pili na hao wanaume nao siku hizi wanawapenda wasichana ambao ni wanafunzi Kweli Kweli. Unashangaa dereva tax kajitokeza huyu sijui wa gari fulani kajitokeza sasa hapo Utakuja kujuta pindi wameshakujua namna mwili wako ulivyo hapo hawatokuwa na hamu na mwingine. Mwanangu sura yako isijeikakufanya unaharibu maisha yako.Kwasababu kwa dunia ya Sasa Jamani kuna magonjwa mengi sana ambayo Kwakweli ukilipata tu hilo gonjwa na ujue kabisaaaaaaa Wewe maisha yako hapo yameshaanza utata tena utata mkubwa sana na mwisho wa siku hadi utashangaa na hadi Ndugu wanakutenga.
Ugonjwa gani huo mama ambao hata ndugu wanafikia kujitenga?.
Ohooooo!!!?. Mwanangu watakutenga na watakutenga kweli kweli na mwisho wa siku majungu tu huko mtaani.Ugonjwa huo moja ya ugonjwa ambao ni  mbaya kabisaaaaaaa ni huu Ugonjwa wa UKIMWI  Yaani mwanangu hapo ukifikia Yaani ni bora hata kupata mimba itajulikana ni namna gani ya kuitoa Au laa ila kwa Hilo gonjwa hapo Kwakweli ni hadi kufa kwako.Kwahiyo ndiyo maana nakuasa sana tangia mwanzoni kwamba mwanangu usitamani Hela ya mtu kwakutegemea kwamba mwili wako ndiyo duka kwamba una bidhaa adimu Sana Lahashaa.Kwasababu mwisho wa siku kama ni bidhaa watanunua na watakuja kuanza kuona kwamba bidhaa zako zimeshapitwa na Wakati tayari.
Sawa mama nimekusikiliza kwa makini sana nanikuahidi mama kuwa sintokuangusha.
Sawasawa ila Chamsingi kama ni maneno yangu nimeshayaongea mda huu hata nikifa leo usiku najua kuna maneno kabisaaaaaaa nilimwachia mwanangu.Basi Sawa embu tufanye kuaandaa Mambo ya chakula naona kama chakula tayari.Kwasababu huyo Baba yako anarudi mda si mrefu kutoka huko msikitini.."mda huo mama Zamda akiwa anaonekana akiwa anakiepua chakula kilichoko jikoni kwakutaka kujua kama kipo tayari"".
Basi ikiwa ni siku iliyofuatia mwanadada Zamda akiwa na rafiki zake wawili ambao Kwakweli huwa anapendana nao kwelikweli. Hao ndiyo marafiki zake wa shuleni.mda huo wakionekana wakiwa ndiyo wanatoka shuleni wakiwa wamevalia sare zao za shule kwa siketi walizokuwa wamevaa ni za rangi ya bluu na mashati kola zao zikiwa zinaonekana ni nyeupe na masweta yakiwa ni ya bluu na chini wakiwa wamevaa viatu vya mwisho saa sita.Basi mda huo nao wakiwa wanaelekea Nyumbani maongezi ya hapa na pale hawayakosi ikiwa ni pamoja na utani ambao Kwakweli uliwafanya wenyewe wawe wanafika nyumbani kwa Haraka sana.Basi mda huo rafiki zake hao mmoja anaitwa Mwantumu na mwingine anaitwa kidawa.Basi mda huo aliyekuwa ameshika Jahazi la kuongea alikuwa ni Zamda. Maongezi yao yalikuwa hivi.
Yaani Kidawa duuu Jana mama kaongea na Mimi kwelikweli hadi nikawa nahisi kweli Sasa kukua shida sijui ni sawasawa na kujitwisha Zigo la chawa Yaani hapo lazima kujikuna kila kona."Mda huo anaongea hivyo hadi akawa anashika kiuno chake ili ainogeshe stori vizuri. Kisha kidogo Kidawa akawa anaingilia mada akiwa anasema ".
Huyo mama yako alikuambia nini Hiyo Jana?."Wote mwendo wakiwa wanatembea mwendo wa Bi Arusi kisha huku Zamda  akawa anasema Hivi".
Yaani shoga WANGU huyo mama kanichachia kweli kweli kuhusiana na Mimi kuvunja ungo. Yaani Hayo maneno ya kiutu ukubwa alivyokuwa akiniambia Yaani sijui tu nisemeje."Mwantumu akawa amedakia mada na kisha akamuuliza Zamda hivi".
Heee Zamda maneno gani tena  Hayo ya kiutu ukubwa wasema .Embu tuambie.
Nakwambia oooo anasema kwamba nijitunze sana kwamba si kila mwanaume akija kunitongoza nimkubalie mwisho wa siku watakuja kuniona kama kopo la maziwa ukishakunywa kopo Hilo thamani yake inashuka kabisaaaaaaa.." kisha Kidawa akarukia maneno ya Zamda kwakusema Hivi ".
Wala hamna cha wakukutema wala nini.Mtoto umejaaliwa umbo Hilo .....mmh..eti....mmh afu wataka kuishi maisha ya kimaskini kwa ubaya gani ulio nao.kuna wenzako wamejaaliwa sura tu Lakini huko nyuma wala.embu check wewe kila mahali Mtoto mashaallah."Kidawa anavyoongea huku kashika kiunio na mwendo kuupunguza ili ampe Zamda vizuri maneno".Yaani kama ndiyo mama yangu ile mwanzoni aliongea Kweli Kweli Kuhusu Mimi kuvunja ungo kuvunja ungo. Wacha weeeee....hayo maneno nakwambia aliyokuwa akinipa utafikiri niko kwenye kicheni part vile kumbe ni mama." mwantumu naye akaunga Mkono kuhusiana na Ushauri wa Kidawa kwa Zamda kwakusema Hivi ".
Kweli Kidawa Mimi mwenyewe mama yangu ananijua nilivyo Yaani Kwaujumla tunajuana naye yaani kila mtu analijua daftari la mwenzake.Mama ile mwanzoni tu Ndiyo Hivyo aliniambiaga tu Mwantumu umeshakuwa karibu ukubwani yanini maneno mengi kama vile wahutubia dunia."Wote walicheka kwa maneno anayoyaongea huyo Mwantumu kwakugonga mikono huku kicheko wakiwa wamenogesha Kwakweli kama vile watu wakubwa kumbe visima vyao ndiyo vimeanzwa kuogelewa na visima vingine ndiyo vinaanza kutafutiwa ni namna gani ya kwenda kuviogelea baada ya kujua ni kisima cha maji ya moto Au ya baridi.Kisha Zamda naye akaamua la kusema".
Mmh....jamani shoga zangu mnavyonitamanisha Yaani ....Yaani sijui nifanyaje tu."Kidawa akarukia mada kwakusema Hivi".
Heeeee wewe nawe ufanyeje wakati kitu kinajulikana hiki ni jambo moja tu la kufanya. "Akiwa anaongea huku akimgusa Zamda".wewe Pale shuleni vile viwalimu usivione tu pale tunavila Hela zao kwelikweli.Wewe unakaje kizembezembe hivyo Wakati una bidhaa asili japokuwa kila msichana anayo Lakini utofauti kwa mwanzoni lazima uwepo."Zamda akamuuliza Kidawa swali hili".
Alafu hao walimu mnakuja kuwalipa nini?." Kidawa na Mwantumu wakacheka kisha Kidawa akasema Hivi".
Zamda hilo ndilo swali kweli. Haya tulia nikujibu kama ifuatavyo. Zamda wewe jiangalie umbo lako kwanza lilivyo afu unasema tawalipa nini.unajifanya unaenda ofisini Lakini huku unatarget zako.afu Sasa haya masketi marefu usiyavaevae sana utakuwa hata hauonekani kama umekuwa shoga wangu. Mbona maisha simple tu.kweli Nyumbani kwetu hawawezikunipa hata hiyo Hela ya bagia afu tena nishindwe kujiongeza Mimi mwenyewe hapa msichana niliyekuwa.Wewe hata huoni tu Zamda sisi na wewe hatufanani wewe uko vizuri kwa umbo ila hauvai vizuri Lakini japokuwa na sisi hatujajaaliwa sana kama wewe Lakini twavaa kisister duuu kwa Sana. Badilika wewe umeshakuwa shoga wangu."Mwantumu naye akaamua kuchangia mada anaongea huku kasimama kajishika kiuno huku akimkodolea macho huyo Zamda.Ilikuwa hivi."
Mimi nikwambie kitu Zamda ushawahi kusikia watu Wanasema kwamba ujana maji ya moto?."Zamda akaitikia kwa kusema ."
Ndiyo nishawahi kusikia ila maana yake halisi sijaipata na sielewi vizuri sana."Kisha Mwantumu akasema Hivi ".
Ahaaaaa kumbe hujui maana yake Basi ndiyo maana unakuwa kama ni mgumu hivi kwenye kuelewa tunachokupanga Hapa. iko hivi tusemapo ujana maji ya moto kwamba kwa umri huu ulionao shoga wangu huu ndiyo umri wakusema kwamba una maji ya moto. Sasa ngojea hayo maji yaje kuwa ya vuguvugu Au baridi haswaaaa Sasa utakuja kujikuta wanaume na wewe ni kama msikiti na mbwa watakavyokuwa wanapita mbali kabisaaaaaaa. Ila kwasasa damu yako bado ni damu ya moto Basi patakuwa ni kama kidonda na nzi haviachani.Tumia ulichojaaliwa wewe."Kisha Zamda ikabidi naye awajibu kwa madaha kwakusema Hivi".
Afu nyiye mashoga zangu msijemkawa mnanisifia tu umbo umbo tu kumbe hata sina nije nianze kujisikia kumbe wala Sina."Mwantumu na Kidawa walicheka kwakusema".
Heheeeeeeeeeeeeeeeeee " Kisha Kidawa akaongea jambo baada ya kucheka kicheko kitamu kwel kweli hadi wanagonga na shoga yake Mwantumu ".  Amakweli kuna mtu unamkuta analalia kitanda cha Kamba na kunguni wanamsumbua Lakini hapo chini ya ardhi yake kuna dhahabu za kutosha. wasamaria wema wanakuambia unadhabu hapo Lakini bado tu hujiamini. Nini Sasa Wakati sisi Ndiyo wataalamu tunajua kwamba vitu kama hivi vya kwako mjini vinauza Kweli Kweli. Nenda na Wakati weeeeee shoga wangu ushakuwa. Yaani Sasa hivi hata ukiwa unamsalimia kijana ukishamuona anaharufu ya vihela vihela Basi tumia ujanja wa kumsalimia na si kila kijana wa kiume anasalimiwa kama unavyomsalimu mama yako Au baba yako.Msalimie kwa mtego.Shoga WANGU Angalia utakuwa unalala njaa na unavaa manguo ya kishamba Shamba tu hapa kumbe kuna Mali unatembea nayo kweli kweli. Kwahiyo shoga yangu Eee Mimi sikundanganyi Kwakweli umejaaliwa Kwahiyo utumie mwili wako vizuri sana hadi utakupatia Fedha.Wewe Zamda mwanzoni Mimi siulikuwa unanionaga navaa manguo Yaani utafikiri naenda kupalilia mahindi afu utafikiri Yaani sijui kama mtu fulani ambaye ni kama kichaa tu.Nikaja kulitambua Hilo jambo kumbe hapa mjini akili na uswahili unahitaji ukishakuwa.Nibaada ya kukalishwa na wataalamu ambao ni maprofessional wamichuno kwa wakaka wale ambao nao wanajifanya fanya kwamba wanahela alafu hawajui namna ya kuzitumia.Yaani baada ya kupita kama wiki moja tu Hivi shoga yangu mbona Hadi maprofessional wamichuno kwa wakaka walinipa saluti. Sasa ndiyo nakushangaa Wewe Hapa. Isijeikiwa tunapigia mbuzi gitaa hapa."Mwantumu naye akamwambia hivi ".
Shoga wangu nikwambie tu kitu sisi ni rafiki zako wakaribu kweli kweli. Kwahiyo unaoona tunakusifia hatukusifii kiunafikinafiki tu hapa. Hapa mjini wewe."Kisha Zamda akawajibu hivi".
Haya shoga zangu acha Mimi niende Nyumbani huyo mama atakuwa ananisubiri kwelikweli niende mtoni.
Hayaaa shogàaaa "Wakajibu kwa pamoja Yaani Kidawa na Mwantumu".
Kwakweli usiku wa siku ile kwa Zamda hata hakusoma Bali akawa anakesha tu akiwa anayachuja mawazo Yaani afuate mawazo ya mama ambayo anajua uchungu wa mwana kwa namna alivyomzaa ai afuate Ushauri wa mashoga zake ambao ni Zamda na Mwantumu.