08-15-2021, 11:24 PM
Si nia niwaumize,kwa hili langu suala
Kuku usimchunguze,kama wataka kumla
Mengi usijiulize,zikajakukifu hila
Kuku ukimchunguza,abadani hutomla
Utengewapo minofu,na michuzi dikodiko
Zifute dhana potofu,kukumbuka atokako
Ukayawaza machafu,kwa yake michakarimo
Kuku ukimchunguza,abadani hutomla
Ni ada kiumbe huyu,kudonoa kuchakua
Kuku sio mbayuwayu,yakupasa kutambua
Mkuyu uwe mbuyu,hapo utajisumbua
Kuku ukimchunguza,abadani hutomla
Shukuru wako Manani,riziki kukupatia
Mkono kwenda kinywani,hii dunia ni njia
Japo atoke jaani,epuka kufuatilia
Kuku ukimchunguza,abadani hutomla
Nyongeza haiwi fungu,hapa mwisho nafikia
Kama hutaki machungu,kaa hili zingatia
Kuku ukimchunguza,abadani hutomla
Abdul Ndembo
Mburahati Sek
Kuku usimchunguze,kama wataka kumla
Mengi usijiulize,zikajakukifu hila
Kuku ukimchunguza,abadani hutomla
Utengewapo minofu,na michuzi dikodiko
Zifute dhana potofu,kukumbuka atokako
Ukayawaza machafu,kwa yake michakarimo
Kuku ukimchunguza,abadani hutomla
Ni ada kiumbe huyu,kudonoa kuchakua
Kuku sio mbayuwayu,yakupasa kutambua
Mkuyu uwe mbuyu,hapo utajisumbua
Kuku ukimchunguza,abadani hutomla
Shukuru wako Manani,riziki kukupatia
Mkono kwenda kinywani,hii dunia ni njia
Japo atoke jaani,epuka kufuatilia
Kuku ukimchunguza,abadani hutomla
Nyongeza haiwi fungu,hapa mwisho nafikia
Kama hutaki machungu,kaa hili zingatia
Kuku ukimchunguza,abadani hutomla
Abdul Ndembo
Mburahati Sek