MyBB Internal: One or more warnings occurred. Please contact your administrator for assistance.
MyBB Internal: One or more warnings occurred. Please contact your administrator for assistance.
MyBB Internal: One or more warnings occurred. Please contact your administrator for assistance.
MyBB Internal: One or more warnings occurred. Please contact your administrator for assistance.
JIFUNZE KISWAHILI - SHAIRI: LEO NADAI TALAKA

JIFUNZE KISWAHILI

Full Version: SHAIRI: LEO NADAI TALAKA
You're currently viewing a stripped down version of our content. View the full version with proper formatting.
LEO NADAI TALAKA
Bwana nilimuamini, mfanowe sielezi,
Kuwa ni mwenye imani, amjuaye Mwenyezi,
Kumbe haikuwa dini, huyu bwana hajiwezi,
Kulala dada na kaka, leo nadai talaka.

Aliniambia hani, ni kufuru kwa Mwenyezi,
Ngoja tufike ndoani, tuianze yetu kazi,
Basi nami sawa hani, nikaacha uchokozi,
Kulala dada na kaka, leo nadai talaka.

Sasa tungali ndoani, imeshapita miezi,
Hakuna kitu chumbani, zaidi ya usingizi,
Jama huyu mume gani, asiyeipenda kazi,
Kulala dada na kaka, leo nadai talaka.

Jambo nimelibaini, haviachi visingizi,
Mara naumwa kichwani, na kubanwa kikohozi,
Ooh nimechoka hani, kama avyo sema juzi,
Kulala dada na kaka, leo nadai talaka.

Havui nguo mwilini, radhi alale na jezi,
Hukishusha kisirani, ati mie mpuuzi,
Niambieni jamani, waume wa siku hizi,
Kulala dada na kaka, leo nadai talaka.

Kumla ninatamani, kwa tamaa sijiwezi,
Mbuzi ina mana gani, kiwa haikuni nazi?
Najiuliza kichwani, mwazani huwa siwazi,
Kulala kaka na dada, leo nadai talaka.

Namkumbuka Mjuni, kijana toka Nyegezi,
Alivyoichanja kuni, kwa kazi hizi mjuzi,
Ni hatari kitandani, kama katoka Shirazi,
Kulala kaka na dada, leo nadai talaka.

Tuachane kwa amani, tusitoane machozi,
Nisemalo ukingoni, yangu mwisho maamuzi,
Twende basi ofisini, niwaambe viongozi,
Kuishi dada na kaka, leo nadai talaka.
Mtunzi Filieda Sanga
Mama B
Mabibo DSM
0753738704