08-07-2021, 11:54 PM
KUPENDA ASOPENDEKA
Paukwa ninatamka,nanyi semeni pakawa
Tungo iweze kufika,musikie sawasawa
Niwaeleze mashaka,moyo uweze kupowa
Kupenda asopendeka,juwa ni kubwa adhabu
Apendwae ajuwapo,kubwa dhiki inakuwa
Takutesa mama popo,upotelewe afuwa
Utaishi kama hupo,huishi kusimbuliwa
Kupenda asopendeka,juwa ni kubwa adhabu
Shemere ya mpendaji,kwa mpendwa ndiko huwa
Lau kama uwe jaji,sheria hupotelewa
Huwa mgonjwa wa uji,hali mzima ingawa
Kupenda asopendeka,juwa ni kubwa adhabu
Kutoka ktk Diwani ya FUTI KAFUTIKA FUTI
Abdul Ndembo
Paukwa ninatamka,nanyi semeni pakawa
Tungo iweze kufika,musikie sawasawa
Niwaeleze mashaka,moyo uweze kupowa
Kupenda asopendeka,juwa ni kubwa adhabu
Apendwae ajuwapo,kubwa dhiki inakuwa
Takutesa mama popo,upotelewe afuwa
Utaishi kama hupo,huishi kusimbuliwa
Kupenda asopendeka,juwa ni kubwa adhabu
Shemere ya mpendaji,kwa mpendwa ndiko huwa
Lau kama uwe jaji,sheria hupotelewa
Huwa mgonjwa wa uji,hali mzima ingawa
Kupenda asopendeka,juwa ni kubwa adhabu
Kutoka ktk Diwani ya FUTI KAFUTIKA FUTI
Abdul Ndembo