MyBB Internal: One or more warnings occurred. Please contact your administrator for assistance.
MyBB Internal: One or more warnings occurred. Please contact your administrator for assistance.
MyBB Internal: One or more warnings occurred. Please contact your administrator for assistance.
MyBB Internal: One or more warnings occurred. Please contact your administrator for assistance.
JIFUNZE KISWAHILI - MISINGI YA HADITHI FUPI (1)

JIFUNZE KISWAHILI

Full Version: MISINGI YA HADITHI FUPI (1)
You're currently viewing a stripped down version of our content. View the full version with proper formatting.
MAELEZO

Utangulizi
Madhumuni ya sehemu hii ni kumsaidia msomaji na mtafiti wa Utanzu wa Badithi fupi na fasihi. Sehemu hii ina mambo ya muhimu yahusuyo Istilahi za Kifasihi, orodha ya vitabu vya hadithi fupi, orodha ya magazeti ambayo yamepata kuchapisha hadithi fupi ama kwa sasa yanaendelea kuchapisha hadithi fupi, Bibliografia na marejeo, orodha ya vitabu vya nadharia ya utanzu wa hadithi fupi na fasihi kwa ujumla ambavyo vimetumika katika kuandaa kitabu hiki.
A. Bibliografia
Hii ni orodha ya makala na vitabu mbalimbali vinavyohusu NADHARIA ya hadithi fupi na fasihi kwa ujumla. Kwa hakika hivi ni baadhi tu ya vitabu ama makala yaliyosomwa katika maandalizi ya kitabu hiki. Bado watafiti wanayo nafasi ya kufanya utafiti mkubwa zaidi.
B. Orodha ya Vitabu vya Hadithi
Kama ilivyoonyeshwa, orodha hii inajumuisha baadhi ya vitabu vya hadithi fupi za aina mbili. Aina ya kwanza ya vitabu hivyo ni ile ambayo inahusu hadithi zile zenye asili ya simulizi, hadithi za kingano.
Hadithi hizi ni fupi sana ukilinganisha na hadithi fupi za kisasa. Aidha, zimepoteza hali yake ya kisanaa kwa kiasi kikubwa kama ilivyojadiliwa katika kitabu hiki katika sehemu ya kwanza.
Kuweko kwa orodha hii ni muhimu kwa sababu hadithi za kisasa zina athari nyingi kutoka hadithi za kingano.
Kundi la pili katika orodha hiyo linahusu hadithi za kisasa. Kulinganisha na kundi la awali, orodha hii si ndefu sana. Hivyo, mwandishi hakuona umuhimu wa kutenganisha orodha hiyo.
C. Orodha ya Magazeti
Magazeti yaliyoandikwa katika orodha hii yana mambo mawili: Kwanza, baadhi ya magazeti hayo kwa sasa hayako. Na yale ambayo yako, mengine hayaandiki tena hadithi fupi kama ilivyokuwa hapo zamani.
Magazeti hayo yamehusika sana katika kukuza lugha ya Kiswahili na kuendeleza hadithi fupi za Kiswahili. Kwa sababu hii orodha hii ni muhimu kwa sababu itawasaidia wapenzi na watafiti wa hadithi fupi za Kiswahili kufanya utafiti zaidi.
D. Istilahi za Fasihi
Hii ni kamusi ndogo ya maneno ya taaluma ya fasihi. Kwa muda mrefu kumekuwa na matumizi mbalimbali ya Istilahi za aina hii. Aidha, mpaka sasa kumekuwa bado na kutoafikiana juu ya matumizi ya baadhi ya Istilahi hizo. Hata hivyo, kuna Istilahi zilizokubalika.
Katika kutayarisha Istilahi hizo ambazo zimetumika humu kitabuni uangalifu mkubwa ulitumika. Istilahi zile zilizokuwa zikitumika na kuzoeleka katika Idara ya Kiswahili ya Chuo Kikuu, Taasisi ya Uchunguzi wa Kiswahili, BAKITA, Vyuoni na katika Shule za Sekondari zimechukuliwa na kutumika vilevile. Kama hakuna Istilahi yoyote iliyopata kutumika, Istilahi mpya irneundwa ili kukidhi haja ya matumizi yake, japo yaweza iwe ni kwa muda tu. Ndiyo kusema kuwa Istilahi hizo zinaweza kubadilika kwa kiasi fulani kadiri siku zipitavyo, lakini tegemeo kubwa ni kuwa nyingi zitabaki na maana zilizoelezwa.
Istilahi nyingi zilizoandikwa katika orodha hii zilipata kujadiliwa na wataalamu mbalimbali katika SEMINA YA FASIHI iliyoandaliwa na Taasisi ya Uchunguzi wa Lugha ya Kiswahili, Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, 1978-79. Aidha, hizi ni baadhi tu ya Istilahi zote zilizoko humo kitabuni. Msomaji anayo nafasi ya kufanya utafiti zaidi na kuongeza idadi ya Istilahi hizo. Ni matumaini ya mwandishi kuwa orodha hii itamsaidia msomaji wa kitabu hiki kuelewa zaidi mambo yaliyojadiliwa humu kitabuni.
E: Faharasa
Huu ni mwongozo wa dhana na mambo muhimu apmoja na majina ya waandishi na wasanii wengine mashuhuri walionukuliwa katika kitabu hiki. Orodha hiyo imeandaliwa kwa uangalifu mkubwa ili kuwafanya wasomaji na watumiaji wa kitabu hiki kwa ujumla wasipate matatizo wanapohitaji kufanya rnarejeo ya haraka.