08-02-2021, 12:14 PM
Ijapo ni jambo tata, hili limejitokeza
Ila sitaficha hata, yote nitayaeleza,
Haya yaliyonikuta, kuhadithia naweza.
Haki alinikamata, hilo shaidi Muweza,
Nilipenda nikadata, pendo alilikoleza,
Nikadhani nimepata, kabisa nikawekeza.
Ila sasa kaniwata, mbali amejisogeza,
Mwingine kapewa ngata, mzigo kuendeleza,
Kasema hawezi juta, chochote hajapoteza.
Niliona pakunata, vibaya nimeteleza,
Hanitaki katakata, na maneno anibeza,
Ni bora angening'ata, kisha angenipuliza.
Kikomo hapa nasema, sioni cha kuniliza,
Ijapo wangu mtima, vibaya kauumiza,
Wacha nienda salama, katu sitayalipiza.
Mshairi Machinga,
mfaumehamisi@gmail.com,
+255716541703/752795964,
Dar es salaam, Kkoo.
Ila sitaficha hata, yote nitayaeleza,
Haya yaliyonikuta, kuhadithia naweza.
Haki alinikamata, hilo shaidi Muweza,
Nilipenda nikadata, pendo alilikoleza,
Nikadhani nimepata, kabisa nikawekeza.
Ila sasa kaniwata, mbali amejisogeza,
Mwingine kapewa ngata, mzigo kuendeleza,
Kasema hawezi juta, chochote hajapoteza.
Niliona pakunata, vibaya nimeteleza,
Hanitaki katakata, na maneno anibeza,
Ni bora angening'ata, kisha angenipuliza.
Kikomo hapa nasema, sioni cha kuniliza,
Ijapo wangu mtima, vibaya kauumiza,
Wacha nienda salama, katu sitayalipiza.
Mshairi Machinga,
mfaumehamisi@gmail.com,
+255716541703/752795964,
Dar es salaam, Kkoo.