MyBB Internal: One or more warnings occurred. Please contact your administrator for assistance.
MyBB Internal: One or more warnings occurred. Please contact your administrator for assistance.
MyBB Internal: One or more warnings occurred. Please contact your administrator for assistance.
MyBB Internal: One or more warnings occurred. Please contact your administrator for assistance.
JIFUNZE KISWAHILI - MAMBO YANAYOSABABISHA KUTOKEA KWA REJESTA

JIFUNZE KISWAHILI

Full Version: MAMBO YANAYOSABABISHA KUTOKEA KWA REJESTA
You're currently viewing a stripped down version of our content. View the full version with proper formatting.
MAMBO YANAYOSABABISHA KUTOKEA KWA REJESTA
(i) Ubinafsi
Ubinafsi ni tabia aliyonayo mtu, iwe ya muda au ya kudumu. Kila mtu ana namna ya kusema na kuandika au kuzungumza, ambayo humtofautisha na watu wengine. Hali hii huleta ubinafsi katika sauti yake (matamshi), msamiati, maandishi yake na mwisho huleta mtindo wa kipekee ambao ni tofauti na watua wengine. Hii ni sababu ya kwanza inayosababisha rejesta katika lugha. Hapa tunapata rejesta za watu.
(ii) Maingiliano
Makundi ya watu mbalimbali yanapochangamana husababisha mwingiliano miongoni mwao. Na ili kuweza kutofautisha kundi moja na kundi jingine kuna mambo fulani fulani ambayo hutofautiana miongoni mwa makundi hayo na mambo haya huweza kuwa ya kipekee katika kundi moja tu. Mambo hayo katika lugha huhusisha matamshi ya maneno, sarufi (mpangilio wa maneno) n.k. Tofauti hizi husababisha mitindo miwili tofauti miongoni mwa makundi hayo – hivyo husababisha kuzuka kwa rejesta.
(iii) Kupita kwa Wakati
Kila mahali katika jamii, hujitokeza mitindo katika kipindi maalumu. Na hii ni kutokana na mabadiliko ya kihistoria yanayoikumba jamii fulani. Kila kipindi cha mpito wa kihistoria huweza kuwa na maneno yake ambayo huwa ni tofauti na kipindi kingine cha kihistoria. Vilevile mitindo ya lugha kutoka kipindi kimoja hadi kipindi kingine huweza kuwa tofauti. Hivyo, rejesta huweza kutokea kati ya kipindi kimoja na kipindi kingine. Mfano, kipindi cha enzi za Ukoloni na kile cha Uhuru, kipindi cha enzi za Azimio la Arusha na kile cha Hali Ngumu ya Maisha au, na kile cha Mfumo wa Mageuzi.
(iv) Shughuli Iliyopo
Hapa hutegemea ni mazingira gani ambapo shughuli hiyo inafanyikia. Mfano misikitini, makanisani, dansini, bandarini, mahakamani, shuleni, nk. Shughuli fulani katika mazingira fulani hutupatia rejesta za mahali.
(v) Tofauti za Hadhi za Wahusika (Uhusiano wa Wahusika)
Mfano wasomi/wasiosoma, mwajiri/mwajiriwa, tajiri/maskini. Hii hali kwa ufupi husababishwa na matabaka yaliyopo katika jamii, tabaka moja na tabaka jingine hutumia lugha ambayo huwa ni tofauti miongoni mwao, na hivyo husababisha rejesta kuzuka miongoni mwa matabaka hayo.
(vi) Matumizi ya Uficho/Tafsida
Hali hii pia husababisha kuzuka kwa rejesta kwani husababisha mitindo mbalimbali ya lugha miongoni mwa wazungumzaji. Kwa mfano vijana wanaweza kutumia maneno haya “silaha yake haina risasi, silaha yake ni butu, silaha yake haiwezi kukata hata kipande cha mkate” wakimaanisha kwamba “uume wake haufai”.
Au
Vijana wa mitaani huweza kusema “Yule anti ni mkarimu kweli kweli, ni mama huruma – anawahudumia vijana wengi, huwashibisha kwa kuwalisha chakula kinono kweli kweli”–wakimaanisha “binti ambaye akitongozwa humkubali kila mwanamme.”
ZINGATIA
Rejesta ni mtindo wa lugha inayotumika mahali penye shughuli fulani ambayo ni tofauti na lugha ya kawaida. Rejesta ya wavuvi, ya washairi, ya wafanyabiashara, ya wahuni, n.k. ni baadhi tu ya mifano. Rejesta zinazotokana na umri, kwa mfano, vijana wana rejesta yao, na wazee wana yao.
Rejesta inayotokana na jinsia, kwa mfano, wanawake wana rejesta yao mbali na ile ya wanaume.
Rejesta zinazohusu watu ni yale mawasiliano yasiyo rasmi ni yalemaongezi ya kawaida ya kila siku au mazungumzo rasmi;
kwa mfano mazungumzo kati ya:
– Vijana wenye rika moja,
– Wazee wenyewe,
– Wanawake wenyewe,
– Wanaume wenyewe,
– Mwalimu na Mwanafunzi,
– Meneja na Wafanyakazi wake,
– Mtu na Mpenzi wake, n.k.
– Marafiki nao wana rejesta yao.
– Rejesta ya mitaani au vijiweni. n.k.