MyBB Internal: One or more warnings occurred. Please contact your administrator for assistance.
MyBB Internal: One or more warnings occurred. Please contact your administrator for assistance.
MyBB Internal: One or more warnings occurred. Please contact your administrator for assistance.
MyBB Internal: One or more warnings occurred. Please contact your administrator for assistance.
JIFUNZE KISWAHILI - DHIMA YA DAYALOJIA/MAJIBIZANO KATIKA KAZI ZA FASIHI

JIFUNZE KISWAHILI

Full Version: DHIMA YA DAYALOJIA/MAJIBIZANO KATIKA KAZI ZA FASIHI
You're currently viewing a stripped down version of our content. View the full version with proper formatting.
Eleza dhima ya dayalojia katika kazi za fasihi ukitoa hoja madhubuti.
Katika kazi za Fasihi dayalojia hutumiwa zaidi katika tamthiliya ingawa hujitokeza pia katika kazi za Fasihi kama riwaya. Utokeaji wa dayalojia hufanya kipengele hiki kionekane kuwa na umuhimu wa pekee na kuleta ulazima wa kuchambua umuhimu wake. Umuhimu wa dayalojia ni kama ufuatao:
  1. Husaidia kuitambulisha kazi ya Fasihi kuwa ni tamthiliya kwa msingi wa ki-Aristotle tamthiliya ni lazima itawaliwe na majibizano (dayalojia).
  2. Kuiwezesha kazi ya tamthiliya kuigizika jukwaani kwa sababu tamthiliya zote ni sanaa za maonesho hivyo ni lazima ziwe katika majibizano ili kuweza kuwapata waigizaji.
  3. Kuipa kazi ya Fasihi muundo wa kimgogoro ambao utaonesha msuko wa visa kimgogoro na kubainisha kwa urahisi chanzo cha mgogoro, kukua kwa mgogoro, kilele cha mgogoro, kushuka kwa mgogoro na suluhisho la mgogoro.
  4. Dayalojia husaidia kuleta uhalisia wa matukio yanayofikishwa na mtunzi, kwa mfano kupitia majibizano ya wahusika tunaweza kubaini hali halisi iliyopo ndani ya jamii kwa urahisi kama inavyojitokeza kupitia “Mama Suzi” na “Baba Joti” wanaoamini kuwa dini na mila haziruhusu kuzungumzia masuala ya mahusiano ya kimapenzi kwa watoto huku “Baba Anna” na “Mjomba” wakiamini juu ya utoaji wa elimu. Lakini pia dayalojia kati ya “Jirani” na “Baba Joti” inasaidia kugundua jinsi wanajamii wasivyoamini juu ya kuwepo kwa janga la UKIMWI na badala yake wanaamini kwenye nguvu za kishirikina.
  5. Dayalojia pia hutumika kuishirikisha hadhira na kuifikirisha kwa kuvaa uhusika kupitia majibizano ya wahusika anaowasoma katika kitabu.
  6. Dayalojia husaidia kupambanisha fikra na mitazamo tofauti ndani ya jamii ambayo kimsingi huathiri mwelekeo mzima wa jamii kujiletea maendeleo kwa ufano imani potofu juu ya malezi ya vijana waliozama katika kizazi cha utandawazi dhidi ya malezi ya vijana wa zama za kale ambao walitishwa kwa miiko ya kijamii tu na wakatii. Hapa unaona wanachoamini “Baba Joti” na “Mama Suzi” dhidi ya wanachokiamini “Mjomba”na “Baba Anna” kuhusu malezi na haja ya jamii kubadili mbinu za malezi ili kuendana na jamii ya sasa.
Kwa ujumla dayalojia ni kipengele muhimu sana katika kazi ya Fasihi hasa tamthiliya kwani pamoja na mambo mengine lakini hipa uhalisia zaidi kazi ya Fasihi na kuchochea tafakari ya mambo yalivyo katika jamii.