MyBB Internal: One or more warnings occurred. Please contact your administrator for assistance.

JIFUNZE KISWAHILI - UUNDAJI WA NOMINO

JIFUNZE KISWAHILI

Full Version: UUNDAJI WA NOMINO
You're currently viewing a stripped down version of our content. View the full version with proper formatting.
Katika mofolojia ya Kiswahili nomino zinaundwaje? Fafanua kwa majibu yako kwa mifano
MAJIBU
 
Kuna taratibu mbalimbali zinazotumika katika kuunda nomino. Baadhi yake ni kama vile:
 
▪ Kuongeza kiambishi mwanzoni mwa kitenzi.
 
Mifano:
 
– (Ku)taka: mtaka
 
– (Ku)tema: mtema
 
– (Ku)tafiti: mtafiti
 
– (Ku)asi: mwasi
 
▪ Kuongeza viambishi mwishoni mwa kitenzi
 
Mifano:
 
– (Ku)badili: badiliko
 
– (Ku)abiri: abiria
 
– (Ku)afiki: afikiano
 
▪ Kubadilisha kiambishi mwishoni mwa vitenzi.
 
Mifano:
 
– (Ku)bikiri: bikira
 
– (Ku)hudumu: huduma
 
– (Ku)faidi: faida
 
– (Ku)fedhehi: fedheha
 
▪ Kubadilisha viambishi katikati ya kitenzi.
 
Mifano:
 
– (Ku)haribu: har«a»bu
 
– (Ku)safiri: sa«fa»ri
 
▪ Kutobadilisha chochote.
 
Mifano:
 
– (Ku)dai: dai
 
– (Ku)hesabu: hesabu