MyBB Internal: One or more warnings occurred. Please contact your administrator for assistance.
MyBB Internal: One or more warnings occurred. Please contact your administrator for assistance.
MyBB Internal: One or more warnings occurred. Please contact your administrator for assistance.
MyBB Internal: One or more warnings occurred. Please contact your administrator for assistance.
JIFUNZE KISWAHILI - NADHARIA MAHUSUSI ZA TAFSIRI

JIFUNZE KISWAHILI

Full Version: NADHARIA MAHUSUSI ZA TAFSIRI
You're currently viewing a stripped down version of our content. View the full version with proper formatting.
 1.Nadharia ya Usawe wa Kimuundo; nadharia hii inatetewa na mtaalam Catford (1969), Tunapofanya kazi ya kutafsiri tunatakiwa kuzingatia ulinganifu wa kimuundo kati ya matini chanzi na matini lengwa, maana yake ni kwamba muundo wa matini chanzi ujitokeze katika matini lengwa. katika nadharia hii muundo ni muhimu. Pia nadharia hii hutumika zaidi katika kutafsiri maandiko ya kidini hasa Biblia.
2. Nadharia ya Usawe wa Kidhima; wa tetezi wa nadharia hii ni pamoja na Nida (1964) na Nida na Taber (1969) wanaona kuwa usawe wa kidhima ni muhimu zaidi kuliko usawe wa kimuundo. Wafasiri wanapaswa kuhakikisha kwamba dhima ya matini chanzi pamoja na athari zake zinajitokeza katika matini lengwa. Yaani kama matini chanzi inawalenga watoto inapaswa iandikwe kiasi kwamba watoto wataweza kuelewa. Pia kwa kuzingatia nadharia hii unapaswa kutumia lugha rahisi na inayoeleweka na watu wote. Vilevile tafsiri yako iwe nzuri kiasi kwamba mtu atakaposoma asiweze kujua kwamba hii kazi imetafsiriwa.
3.Nadharia ya Usawe wa Aina-matini; matini yoyote ile ifasiriwe kwa kuzingatia aina yake. Hii inamaana kwamba kazi itakayotokea itafanana na matini chanzi. Kma matini chanzi ni ya kisheria itakapotafsiriwa matini lengwa nayo itaonekana kuwa ya kisheria. Katika nadharia hii kinachozingatiwa ni fani (muundo) na maudhui (dhima/lengo) ya matini yenyewe inayotafsiriwa. Watetezi wa nadharia hii ni Reiss (1971),  Buhler (1965) na Newmark (1982/88)
4.Nadharia Changamani (Cross Fertilization theory). Hii ni nadharia tete iliyoasisiwa na P.S.Malangwa (2010) Ndharia hii inadai kwamba huwezi kufanya tafsiri kwa kutumia nadharia moja tu, kwa sababu hakuna nadharia inayojitosheleza yenyewe.