MyBB Internal: One or more warnings occurred. Please contact your administrator for assistance.
MyBB Internal: One or more warnings occurred. Please contact your administrator for assistance.
MyBB Internal: One or more warnings occurred. Please contact your administrator for assistance.
MyBB Internal: One or more warnings occurred. Please contact your administrator for assistance.
JIFUNZE KISWAHILI - VIGEZO VINAVYOSABABISHA UGUMU WA KUJIFUNZA LUGHA YA PILI

JIFUNZE KISWAHILI

Full Version: VIGEZO VINAVYOSABABISHA UGUMU WA KUJIFUNZA LUGHA YA PILI
You're currently viewing a stripped down version of our content. View the full version with proper formatting.
Vigezo vinavyosababisha ugumu wa kujifunza lugha ya pili
Hivyo vipengele vitano vinavyojitokeza kurahisisha kujifunza lugha-mama huwa vigumu
kupatikana katika kujifunza lugha ya pili, yaani mazingira, muda, walimu,
mwingiliano na lugha nyingine, uhusiano na wengine.
Mwingiliano wa lugha-mama na lugha ya pili ni kigezo kikubwa sana. Mwanafunzi wa makabila
mbalimbali wanashindwa kukimudu Kiswahili kutokana na athari za lugha-mama zao.
Kuna matatizo ya:
(a) Kuchanganya sauti au kubadili sauti k.m. chai (wanyakyusa) kyai
(b) Kuondoa sauti k.m. halafu (wahaya) alafu
© Kuongeza sauti k.m. mtu (wajaluo) mutu
(d) Kubadili sauti k.m. thelathini (wasambaa) selasini
Kila mtoto mwenye akili timamu anamudu vizuri sana lugha-mama yake. Lakini inapofika lugha ya pili panajitokeza matatizo mengi. Tutawezaje kupunguza matatizo hayo?
Kwanza, kujitahidi kufuata kanuni zile za kujifunza lugha ya kwanza zinazowezekana k.m. kusikiliza na kuzungumza kutangulie; kisha kusoma na kuandika.
Pili, ufundishaji ya lugha ya pili pia uwe katika mazingira halisi. Mwalimu ujitahidi kutengeneza mazingira halisi na kutumia mifano dhahiri. Kama vitu dhahiri kama nyoka, waziri n.k. haviwezi kuletwa darasani basi picha na michoro dhahiri itumike.
Tatu, mwalimu utoe mazoezi mengi na ya mara kwa mara. Mazoezi hayo yatajumuisha stadi zote za kusikiliza, kuzungumza, kusoma na kuandika.
Nne, katika kufanikisha kujifunza lugha ya pili, itabidi kuwa na marudio ya mara kwa mar. hii itasaidia kujenga uzoefu na hivyo kuimarisha uzingatiaji.