MyBB Internal: One or more warnings occurred. Please contact your administrator for assistance.

JIFUNZE KISWAHILI - Vitenzi vya Silabi Moja

JIFUNZE KISWAHILI

Full Version: Vitenzi vya Silabi Moja
You're currently viewing a stripped down version of our content. View the full version with proper formatting.
Vitenzi vya Silabi Moja
Hivi ni vitenzi vyenye silabi moja pekee. Ili kuleta maana kamili, vitenzi hivi huambatanishwa na kiungo KU- katika kauli ya kutenda. Kama vitenzi vingine, vitenzi vya silabi moja vinaweza kunyambuliwa. k.m: soma, kula, sikiza
  1. -cha - kucha - jua linapochomoza asubuhi k.m kumekucha

  2. -fa - kufa - kuacha kupumua, kupoteza uhai k.m amekufa

  3. -ja- kuja - fika mahali hapa k.m nimekuja

  4. -la- kula - kutia chakula mdomoni k.m anakula

  5. -nya- kunya - kutoa mabaki ya chakula toka tumboni k.m mtoto amekunya

  6. -nywa- kunywa - kutia kinywaji kama vile maji au maziwa mdomoni k.m ninakunywa uji

  7. -pa- kupa - kumkabithi/kumpatia mtu kitu k.m amenipa pesa

  8. -pwa- kupwa - kujaa hadi pomoni - k.m kisima kimekupwa maji

  9. -twa- kutwa - jua linapozama magharibi na usiku kuingia k.m kumekutwa

  10. -wa- kuwa - kutokea katika hali au mahali fulani k.m alikuwa