MyBB Internal: One or more warnings occurred. Please contact your administrator for assistance.

JIFUNZE KISWAHILI - ETIMOLOJIA YA NENO "DAFRAO''

JIFUNZE KISWAHILI

Full Version: ETIMOLOJIA YA NENO "DAFRAO''
You're currently viewing a stripped down version of our content. View the full version with proper formatting.
HII NDIYO ETIMOLOJIA YA NENO "DAFRAO''

Neno *dafrao* katika lugha ya Kiswahili ni *nomino: [Ngeli: i-/zi-*] yenye maana zifuatazo:

1. Tukio la kugongana uso kwa uso kwa vyombo vinavyotembea.

2. Chuma kigumu kinachofungwa Mbele ya gari ili kuzuia uharibifu wakati magari yanapogongana.

Neno hili *dafrao* linatokana na neno la Kiarabu *dafraau دفراء* na lenye maana zifuatazo:

1.  Kilichodhalilika.

2. Kitu kilichooza, kikanuka na kutoa wadudu.

3. Aina ya mmea wa kitropiki. Kwa Kiingereza huitwa *scoparia.*

Kinachodhihiri ni kuwa neno *dafraau  دفراء* lilipoingia katika Kiswahili na kutoholewa kuwa neno *dafrao* maana yake kati lugha ya asili - Kiarabu ilibadilika na kupata maana mpya zilizotajwa.

*Shukran sana.*

*Khamis S.M. Mataka.*