MyBB Internal: One or more warnings occurred. Please contact your administrator for assistance.

JIFUNZE KISWAHILI - ETIMOLOJIA YA NENO "BULIBULI''

JIFUNZE KISWAHILI

Full Version: ETIMOLOJIA YA NENO "BULIBULI''
You're currently viewing a stripped down version of our content. View the full version with proper formatting.
HII NDIYO ETIMOLOJIA YA NENO "BULIBULI''

Neno *bulibuli* katika lugha ya Kiswahili ni *nomino: [Ngeli: i-/zi-*] yenye maana ya mtindo mmojawapo wa kofia nyeupe yenye nakshi (viua) inayovaliwa hasa mwambao wa pwani ya Afrika Mashariki, kofia ya kazi.

Pia ni kivumishi kwa maana ya: -zuri, -a kupendeza, bambam, -ema.

Mwanafunzi mwenye tabia bulibuli hufaulu vizuri katika mitihani yake.

Katika lugha ya Kiarabu, neno hili *bulibuli* linatokana na nomino ya Kiarabu *bulbulu بلبل* yenye maana zifuatazo:

1. Ndege mdogo aina ya kunega maarufu kwa kuimba vizuri.

2. Sehemu ya kumiminia maji katika birika.

Kinachodhihiri ni kuwa neno *bulbulu  بلبل* lilipoingia katika Kiswahili na kutoholewa kuwa neno *bulibuli* lilichukua maana mpya ya (nomino) kofia yenye viua inayovaliwa pwani ya Afrika Mashariki na maana ya (kivumishi): -zuri, -a kupendeza, bambam, -ema.

*Shukran sana.*

*Khamis S.M. Mataka.*