MyBB Internal: One or more warnings occurred. Please contact your administrator for assistance.

JIFUNZE KISWAHILI - ETIMOLOJIA YA NENO "BUGHUDHA''

JIFUNZE KISWAHILI

Full Version: ETIMOLOJIA YA NENO "BUGHUDHA''
You're currently viewing a stripped down version of our content. View the full version with proper formatting.
HII NDIYO ETIMOLOJIA YA NENO "BUGHUDHA''

Neno bughudha katika lugha ya Kiswahili ni nomino: [Ngeli: i-/zi-] yenye maana ya mambo yanayomkasirisha au kumuudhi mtu, maneno na vitendo vinavyomfanya mtu audhike.

Katika lugha ya Kiarabu, neno hili bughudha linatokana na tendo-jina la Karabu bugh-dhwun بغض lenye maana ya chuki linalotokana na kitenzi cha Kiarabu baghadhwa (soma: baghadhwa/yabghadhwu/bugh-dhwan بغض، يبغض، بغضا)  chenye maana zifuatazo:

1. Kuchukia.

2. Kuchukiza.

3. Kuchukiwa.

Kinachodhihiri ni kuwa neno bugh-dhwun  بغض lilipoingia katika Kiswahili na kutoholewa kuwa neno bughudha lilichukua maana mpya ya maneno na vitendo vinavyomfanya mtu audhike, mambo yanayomkasirisha au kumuudhi mtu.

Shukran sana.

Khamis S.M. Mataka.