MyBB Internal: One or more warnings occurred. Please contact your administrator for assistance.

JIFUNZE KISWAHILI - ETIMOLOJIA YA NENO SHUKURANI ''

JIFUNZE KISWAHILI

Full Version: ETIMOLOJIA YA NENO SHUKURANI ''
You're currently viewing a stripped down version of our content. View the full version with proper formatting.
HII NDIYO ETIMOLOJIA YA NENO SHUKURANI ''

Neno *shukurani* katika lugha ya Kiswahili ni *nomino: [Ngeli: i-/zi-*] yenye maana ya maneno yanayotolewa kuonesha kuupokea kwa mikono miwili wema uliotendewa; *ahsante/asante.*

*Nahau* : *Toa shukurani:* sema ahsante.

Katika lugha ya Kiarabu, neno hili *shukurani* limechukuliwa kutoka neno la Kiarabu  *'shukraan* *(soma: shukraanun/shukraanan/shukraanin  شكران)**  tendo-jina  *Masdar مصدر* la *kitenzi* cha Kiarabu *shakara شكر* chenye maana zifuatazo:

1. Amemsifu na kumtaja mtu mwengine kwa wema kutokana na hisani aliyomfanyia.

2. Amemlipa mtu mwengine malipo fulani kwa kuifanya vizuri kazi aliyomtuma.

Kinachodhihiri ni kuwa neno la Kiarabu *'shukraanun  شكران*  lilipoingia katika Kiswahili na kutoholewa kuwa neno *shukurani* halikubadili maana katika lugha ya Kiarabu.

*Shukran sana.*

*Khamis S.M. Mataka.*