MyBB Internal: One or more warnings occurred. Please contact your administrator for assistance.

JIFUNZE KISWAHILI - ETIMOLOJIA YA NENO 'BALAGHAMU/BELGHAMU'

JIFUNZE KISWAHILI

Full Version: ETIMOLOJIA YA NENO 'BALAGHAMU/BELGHAMU'
You're currently viewing a stripped down version of our content. View the full version with proper formatting.
HII NDIYO ETIMOLOJIA YA NENO 'BALAGHAMU/BELGHAMU'

Neno *balaghamu/belghamu* katika lugha ya Kiswahili ni *nomino: [Ngeli: li-/ya-*] yenye maana ya kioevu kizito kilichochanganyika na utandoute kinachotolewa kwa wingi kwa njia ya kupumulia hususan mtu anapougua mafua au kikohozi, mate mazito yanayokuwa kooni ambayo hutoka mtu anapokohoa.

*Msemo:* *Toa balaghamu zako*: toa hasira zako.

Katika lugha ya Kiarabu, neno hili *balaghamu/belghamu* limechukuliwa kutoka neno la  Kiarabu  *'balghamu* *(soma: balghamun/balghaman/balghamin  بلغم)**  lenye maana ya mate yaliyochanganyika na kamasi na hutoka kwa njia ya upumuaji, dutu laini ya mate iliyochanganyika na kamasi; *kohozi*.

Kinachodhihiri ni kuwa neno *'balghamun بلغم* lilipoingia katika Kiswahili na kutoholewa kuwa neno *balaghamu/belghamu* halikubadili maana katika lugha asili- Kiarabu.

*Shukran sana.*

*Khamis S.M. Mataka.*