MyBB Internal: One or more warnings occurred. Please contact your administrator for assistance.
MyBB Internal: One or more warnings occurred. Please contact your administrator for assistance.
MyBB Internal: One or more warnings occurred. Please contact your administrator for assistance.
MyBB Internal: One or more warnings occurred. Please contact your administrator for assistance.
JIFUNZE KISWAHILI - MAANA YA METHALI

JIFUNZE KISWAHILI

Full Version: MAANA YA METHALI
You're currently viewing a stripped down version of our content. View the full version with proper formatting.
MAANA YA METHALI
Wataalamu mbalimbali wamejaribu kutoa fasili ya maana ya methali. Mazrui na Syambo (1992), methali ni misemo mifupi yenye hekima fulani. Wamesisitiza kuwa methali hudhihirisha mkusanyiko wa mafunzo waliyopata watu wa vizazi vingi vya jumuiya wanayoishi katika maisha yao. Aidha, wameongeza kusem kuwa methali ni sehemu moja ya lugha inayoweza kubaini falsafa ya watu fulani kuhusu maisha kwa ujumla.
Ngole na Honero (1981), wamesema kuwa methali ni aina ya usemi mzito na ambao unakusudiwa kusema jambo maalumu kwa njia ya fumbo. Methali hukusudiwa kumuonya, kumuongoza na kumuadilisha mwanadamu katika maisha yake. Aidha, kwa umbile la nje methli huwa na muundo wa pande mbili. Upande mmoja wa methali hueleza mazoea au tabia ya watu au kitu katika utendaji wa jambo. Upande wa pili wa methali hueleza matokeo yaliyosababishw na mazowea au tabia iliyoelezwa katika upande wa kwanza.
Murega (2015), ameona kuwa methali ni semi fupi ya kimapokeo yenye muundo mahsusi na iliyo na fumbo amblo linapofasiliwa  hupata maana mbalimbali hutegemea muktadha na hali halisi ya maisha ya watumiaji.
Wamitila (2001), ameeleza kuwa methali ni msemo unaojitosheleza, wenye maana yenye nguvu au uzito, wenye muundo au sifa za kishairi, unaokusudiwa kuadibu au kuelekeza, kuelimisha, kushauri na kadhalika.
Kutokana na fasili za wataalamu hao, tunaweza kusema kuwa methali ni aina ya usemi mzito unaoelezea wazo pana kwa muhtasari ukiwa na umbo mahsusi na unaotumia uzowefu wa jamii kuonya, kuadilisha na kufunza kwa kuzingatia miktadha maalumu. Methali hutumia hekima, uficho wa kauli, usanii w kimsamiati, uzowefu wa matukio katika jamii na falsafa ya jamii katika mitazamo ya masuala mbalimbali ambayo huakisi maisha na utamaduni wa jamii husika.