MyBB Internal: One or more warnings occurred. Please contact your administrator for assistance.

JIFUNZE KISWAHILI - ETIMOLOJIA YA NENO 'BASHASHA'

JIFUNZE KISWAHILI

Full Version: ETIMOLOJIA YA NENO 'BASHASHA'
You're currently viewing a stripped down version of our content. View the full version with proper formatting.
HII NDIYO ETIMOLOJIA YA NENO 'BASHASHA'

Neno *bashasha* katika lugha ya Kiswahili ni *nomino: [Ngeli: i-/zi-*] yenye maana zifuatazo:

1. Hali ya kuonesha furaha; ucheshi, uchangamfu.

2. Furaha na uchangamfu.

*Mfano:* Mgeni rasmi alipokelewa kwa bashasha kubwa.

Katika lugha ya Kiarabu, neno hili *bashasha* limechukuliwa kutoka neno la Kiarabu  *'bashaasha* *(soma: bashaashatun/bashaashatan/bashaashatin  بشاشة)**  lenye maana zifuatazo:

1. Tendo-jina *masdar  مصدر* la kitenzi cha Kiarabu *bash-sha  بش* chenye maana ya: *amekunjua uso wake, amemfurahikia aliyekutana naye, amempa faraja.*

2. Hali ya kumlaki mtu kwa furaha na kicheko.

3. Uso mkunjufu uliojaa furaha na tabasamu. 

Kinachodhihiri ni kuwa neno *'bashaashatun بشاشة* lilipoingia katika Kiswahili na kutoholewa kuwa neno *bashasha* halikubadili maana yake katika lugha asili- Kiarabu.

*Shukran sana.*

*Khamis S.M. Mataka.*