MyBB Internal: One or more warnings occurred. Please contact your administrator for assistance.

JIFUNZE KISWAHILI - ETIMOLOJIA YA NENO 'KALIBU'

JIFUNZE KISWAHILI

Full Version: ETIMOLOJIA YA NENO 'KALIBU'
You're currently viewing a stripped down version of our content. View the full version with proper formatting.
HII NDIYO ETIMOLOJIA YA NENO 'KALIBU'

Neno *kalibu* katika lugha ya Kiswahili ni *nomino: [Ngeli: i-/zi-*] yenye maana zifuatazo:

1. Chombo kitumikacho kuyeyushia madini kwa mfano risasi.

2. Kifaa chenye umbo maalumu ambacho humiminiwa madini yaliyoyeyushwa ili kupata umbo lake.

3. Jiko la kuchomea saruji.

Neno *kalibu* pia ni *kitenzi elekezi* chenye maana ya ' *tia risasi iliyoyeyushwa katika chombo ili kupata umbo litakiwalo'.*

Katika lugha ya Kiarabu, neno hili *kalibu* limechukuliwa kutoka neno la Kiarabu  *'qaalibu*( *soma: qaalibun/qaaliban/qaalibin قالب )* ambalo ni nomino ya Kiarabu yenye maana zifuatazo:

1. Kifaa kinachomiminiwa johari au madini au kitu chochote kilichoyeyushwa ili kupata umbo lake.

2. Kitu kutokana na chuma au mti kinachowekwa ndani ya kiatu cha ngozi ili kukinyoosha na kukilainisha

3. Ndege tai mwekundu.

4. Mtoto wa mbuzi ambaye hakuchukua rangi ya mama yake.

Kinachodhihiri ni kuwa neno *'qaalibun قالب* ambalo katika Kiarabu huitwa pia *qaalabun* lilipoingia katika Kiswahili na kutoholewa kuwa neno *kalibu* halikubadili maana yake katika lugha ya Kiarabu ingawa liliacha maana zingine.

*Shukran sana.*

*Khamis S.M. Mataka.*